RAIS WA ZANZIBAR DK.MWINYI ATEMBELEA MRADI WA NYUMBA ZA MAAFA TUMBE WILAYA YA MICHEWENI PEMBA. |Shamteeblog.

 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akitembelea moja ya Nyumba za Maafa Tumbe akipata maelezo ya Mradi huo kutoka kwa Katika Mkuu Ofisi  ya Makamu wa Pili wa Rais Sera Uratibu na Baraza la Wawakilishi Ndg. Thabit Idarous Faina, alipofanya ziara kutembelea Mradi huo.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Muuguzi Mkuu Pemba Daktari.Omar Juma Ali akitowa maelezo ya Kituo cha Afya kilichoko katika eneo hilo la Nyumba za Maafa Tumbe, Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba, alipofanya ziara kutembelea Mradi huo.(Picha na Ikulu)

BAADHI ya Nyumba za Maafa katika Kijiji cha Tumbe Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba zilizojengwa kwa ajili ya Wananchi watakaopata na maafa Kisiwani Pemba.(Picha na Ikulu)

WANANCHI wa Kijiji cha Tumbe Wilaya ya Micheweni wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) akizungumza na Wananchi hao katika viwanja vya Nyumba za Maafa Tumbe alipofika kutembelea ujenzi huo.(Picha na Ikulu)

WANANCHI wa Kijiji cha Tumbe wakishangilia wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akiwahutubia katika viwanja vya Nyumba za Maafa Tumbe Wilaya ya Micheweni alipofika kukagua Mradi huo.(Picha na Ikulu) MZEE wa Kijiji cha Tumbe Shehia ya Magharibi Bw.Juma Kombo Dadi akimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Tumbe wakati alipofika kuangalia maendeleo ya Ujenzi wa Nyumba za Maafa Tumbe Wilaya ya Micheweni Pemba, akiwa amebeba bago la picha za Waasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar.(Picha na Ikulu)

 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi akitembelea Mradi wa Nyumba za Maafa zilizojengwa katika eneo la Kijiji cha Tumbe Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba, akiwa katika ziara yake kukagua maendeleo ya Mradi huo na (kulia kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais. Sera Uratibu na Baraza la Wawakilishi Mhe.Dkt.Khalid Salum Mohammed.(Picha na Ikulu)


By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post