RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akitembelea Kiwanda cha Sukari Mahonda Mkoa wa Kaskazini Unguja akiwa katika ziara yake akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda hicho Ndg. Rahim Bhaloo (kushoto kwa Rais) akitowa maelezo ya uzalishaji wa sukari na (kulia kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud na Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mhe.Omar Said Shabaan.(Picha na Ikulu) RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha Sukari Mahonda Ndg. Rahim Bhaloo (kushoto kwa Rais) akitowa maelezo ya uzalishaji wa Sukari katika kiwanda hicho wakati akiwa katika ziara yake leo na (kulia kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud, Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mhe.Omar Said Shabaan na Waziri wa Kilimo Umwagiliaji Maliasili na Mifugo Mhe.Dkt. Soud Nahoda Hassan.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha Sukari Mahonda Zanzibar,Ndg Rahim Bhaloo, wakati wa ziara yake kutembelea kiwanda hicho kuangalia uzalishaji wa sukari.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akipata maelezo na kuangalia Sukari iliozalishwa na kiwanda hicho kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu Ndg. Rahim Bhaloo, akiwa katika ziara yake kujionea uzalishaji wa Sukari kiwandani hapo leo, 6-3-2021.(Picha na Ikulu) MFANYAKAZI wa Kiwanda cha Sukari Mahonda Ndg. Amour Juma akitowa changamoto zinazowakabili katika Uongozi wa Kiwanda cha Sukari Mahonda, wakati ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) mkutano huo umefanyika katika viwanja vya kiwanda hicho Mahonda Mkoa wa Kaskazini Unguja leo 6-3-2021.(Picha na Ikulu) RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Wafanyakazi wa Kiwanda cha Sukari na Wakulima wa miwa, wakati wa ziara yake kutembelea kiwanda hicho kujionea uzalishaji wa Sukari kiwandani hapo.(Picha na Ikulu)
MKULIMA wa zao la Miwa kutoka Cheju Ndg.Mohammed Omar akizungumza changamoto zao kuhusiana kilimo cha miwa wakati wa ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) mkutano huo umefanyika katika viwanja vya kiwanda hicho mahonda leo 6-3-2021.(Picha na Ikulu) RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akisikiliza changamoto za Wafanyakazi wa Kiwanda cha Sukari Mahonda wakati wa ziara yake kutembelea kiwanda hicho leo 6-3-2021 na (kushoto kwa Rais) Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha Sukari Mahonda Ndg. Rahim Bhaloo.(Picha na Ikulu)
By Mpekuzi
Post a Comment