MKUU wa wilaya ya Karagwe Mhe Godfrey Mheluka kushoto ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Kagera akikabidhi Cheti cha Utambuzi cha Mhe Mbunge Neema Lugangira kwa Katibu wake Kitaifa Judith John leo |
WALIMU Wanawake wakikabidhi kitenge kilichoandikwa "Super Woman"cha Mhe Neema Lugangira kwa Katibu wake Kitaifa Judith John |
CHETI cha Utambuzi na Kitenge cha Super Woman alichopewa Mhe Neema Lugangira na Walimu wa Wanawake wa Bukoba Manispaa |
WALIMU Wanawake wa Manispaa ya Bukoba kupitia kitengo cha walimu Wanawake cha Chama cha Walimu Tanzania (CWT) wamemkabidhi Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) kupitia NGOs Neema Lugangira cheti cha Utambuzi na Sare ya Kitenge kilichoandikwa “Super Woman".
Cheti hicho ambacho kimekabidhiwa leo ikiwa ni siku ya Wanawake Duniani 2021 kinadhihirisha namna walimu hao wanavyothamini juhudi kubwa ambazo zimekuwa zikifanywa na Mbunge Neema Lugangira katika kuchangia Maendeleo ya Jamii wilaya ya Bukoba Mjini.
Akipokea cheti hicho kwa niaba ya Mbunge Neema Lugangira ambaye yupo mjini Dodoma kwa ajili ya Vikao vya Kamati za Bunge,Katibu wa Mbunge huyo Kitaifa Judith John alisema kwamba cheti hizo wamekipata wakati muafaka kutokana na juhudi kubwa zinazonyeshwa na mbunge huyo katika kuhakikisha anawapa maendeleo.
Akizungumzia cheti hicho,Mbunge Neema Lugangira aliwashukuru Walimu Wanawake wa Manispaa ya Bukoba kupitia Kitengo cha Walimu Wanawake cha Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Bukoba Manispaa kwa kutambua juhudi zangu za kuchangia Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Bukoba Mjini .
“Kwa kweli kitendo hiki cha Walimu hapa kunipa Cheti cha Utambuzi na Sare ya Kitenge iliyoandikwa "Super Woman" leo Siku ya Wanawake Duniani 2021 kinaonyesha namna wanavyotambua na kuthamini mchango wangu kwao na nihaidi tutaendelea kushirikiana kuhakikisha wanapata mafanikio makubwa”Alisema .
Hata hivyo pia alimshukuru Mgeni Rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Karagwe, Mhe Godfrey Mheluka aliyekuwamwakilisha Mhe Mkuu wa Mkoa Kagera kwa kumpongeza Mbunge Neema Lugangira na Shirika la Agri Thamani ambalo yeye ni Mkurugenzi kwa namna ambavyo wameendelea kutoa Elimu ya Lishe Bora.
Mbunge Neema aliongeza pia Mkuu huyo wa Wilaya aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa aliwataka waendeleze mapambano kwani Mkoa wa Kagera bado unaongoza kwa idadi halisia kwenye Udumavu
“Bila Lishe hakuna Maendeleo na sisi tunakubaliana naye kabisa hivyo tutahakikisha tunawaunga mkono walimu wote kwa lengo la kuhakikisha tunaondokana na hali hii kuanzia shuleni hadi kwenye jamii", Alisema
Hata hivyo aliwashukuru Walimu Wanawake wa Bukoba Manispaa kwa Utambuzi huo na anawasaidi huku akihaidi kushirikiana nao katika maeneo mbalimbali hususan katika kufanikisha Lishe Shuleni na Hedhi Salama Shuleni
By Mpekuzi
Post a Comment