*Ruangwa 10 zinachangamoto ya Mawasiliano ya simu kupatikana
*Meneja wa Posta abainika kunyanyasa wafanyakazi wenzake.
Na Chalila Kibuda, Lindi
NAIBU Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Andrea amesema kuwa uchumi unakwenda kwa kasi katika sekta ya Mawasiliano hivyo kunahitaji umadhubuti katika uimarishaji wa miundombinu.
Waziri huyo ameyasema katika ziara tofauti alipotembelea Mkoa wa Lindi pamoja na Wilaya za Ruangwa na Nachingwea ,amesema kuwa wadau wa wanaosimamia miundombinu ya Mawasiliano wanatakiwa kujipanga kwenda sambamba na teknolojia kutoka 2G kwenda 4G ambapo kila mwananchi ataweza kutumia data.
Mhandisi Kundo amesema uchumi uliokuwa unategemewa ni ule wa kutumia barabara lakini sasa uchumi huo unakwenda katika mawasiliano ambako ndio dunia iko huko.
Aidha amesema katika kuna malalamiko yako kwa wananchi katika uwekaji minara kwa baadhi ya watu kutumia udanganyifu kwa wananchi hao kwa kununua maeneo ikiwa kama makazi lakini baadaye unaota mnara.
Naibu Waziri Kundo amesema kuwa mkoa wa Lindi Shirika la Mawasiliano (TTCL) na Posta kwenda kiushindani kwani hakuna matokeo yanayoonyesha kufanya vizuri katika Mkoa Lindi.
Aidha amesema kuwa Shirika la Posta kwa Meneja wa Mkoa wa Lindi ananyanyasa wafanyakazi wenzake na kutaka ajirekebishe kwa haraka ambapo wakati wa ziara hiyo hakuwepo kwa madai anaumwa aliyesemewa na mfanyakazi.
Katika Wilaya ya Ruangwa Naibu Waziri huyo amezitaka Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo kushughulikia Kata kumi kuweza kupata mawasiliano kwa kuweka kipaumbele.
Amesema kuwa TTCL wajipange kuchangamkia fursa zilizopo ili kuwa na ushindani wa kibiashara na sio kufanya kazi kwa mazoea ya kutoonekana matokeo chanya katika kuongeza wateja.
Katika Ziara hiyo Wilaya ya Nachingwea Mhandisi Kundo amesema kuwa watoa huduma kufanya utafiti wa kufanya maeneo yanafikiwa na huduma kwani mahitaji ya wananchi wanaongezeka katika kutumia mawasiliano mbalimbali.
Ziara hiyo ilikuwa na Watendaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ,Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) pamoja na wotoa huduma za mawasiliano ya simu za mkononi.
By Mpekuzi
Post a Comment