WAZIRI WA NISHATI DKT MEDADI KALEMANI AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA NJIA YA KUSAFIRISHA UMEME BARIADI |Shamteeblog.
Samirah Yusuph,
Bariadi. Waziri wa nishati Dkt Medadi Kalemani ameweka jiwe la msingi katika ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa kilovolti 220 na kituo cha kupokea na kupoza umeme cha Imalilo wilayani Bariadi Mkoa wa Simiyu wenye gharama ya bilioni 75.
Katika uwekaji wa jiwe hilo Machi 03, Kalemani ameagiza kukamilika kwa mradi huo katika kipindi cha miezi tisa hadi kumi na mbili ili kuwawahishia wananchi huduma ya umeme wa uhakika ambayo ilikuwa haipatikani kwa muda mrefu.
Ambapo amelitaka shirika la umeme nchini Tanesco kuhakikisha kuwa litandaza mtandao wa nguzo za umeme katika maeneo yote vijijini ili kuhakikisha kuwa wananchi wote wanapata umeme majumbani.
"Zoezi la uwekaji wa umeme majumbani kwa sasa sio suala la hiali badala yake ni jambo la lazima ni kila mwananchi awe na umeme katika makazi yake...
Serikali imetumia gharama kubwa kujenga miradi hii hivyo yule atakayeshindwa kuvuta umeme nyumbani kwake tutamtafuta aseme ni kwa nini ameshindwa kuweka umeme".
Aidha aneagiza kuwa Kwa sasa mita zote za umeme katika mitaa na vijiji vitauzwa kwa bei moja bila kujali umbali wa kaya na nguzo hata walio nje ya mita 30 za nguzo watapata umeme kwa bei elekezi ambayo ni tsh 27,000.
Akitoa taarifa ya shirika la umeme mkurugenzi mtendaji wa Tanesco Tito Mwinuka, amesema kuwa ujenzi wa mradi huo umegharimu kiasi cha bilioni 75 pamoja na bilioni 46.7 kwa ajili ya fidia kwa wananchi waliopisha eneo la Mradi.
"Tayari wananchi wameanza kupewa stahiki zao kama fidia baada kupisha mradi huu".
Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Festo Kiswaga amesema kuwa ujenzi wa mradi huo katika Mkoa wa Simiyu utapelekea upatikanaji wa umeme kuwa wa uhakika tofauti na ilivyokuwa awali.
"Uwepo wa umeme wa uhakika katika Mkoa wetu inakwenda kuwa chachu ya kuinua uchumi wa wananchi kwa sababu wananchi wa mkoa huu ni wakulima, kupitia kulimo wataweza kulima kisasa kwa kutumia mashine ambazo zinahitaji Kumia umeme ikiwa ni pamoja na usindikaji wa mazao jambo ambalo litaongeza tija katika kilimo.
Aidha ameongeza kuwa ni wakati wa shirika la umeme kuboresha miundo mbinu ikiwamo nguzo za umeme zilizo choka ili kuhakikisha umeme haukati mara kwa mara na kuwapa adha wananchi.
Hapo awali Mkoa wa Simiyu haukuwa na kituo cha kupoza, kupokea na kusafirisha umeme badala yake ulipokea umeme kutoka katika vituo vya kupozea umeme kutoka Mwanza na Shinyanga kwa sasa kituo hiki kitakuwa na uwezo wa kufua kilowati 100 za umeme mara mbili ya hitaji la umeme kwa Mkoa.
Mwisho.
By Mpekuzi
Post a Comment