Benki ya Exim imesisitiza kuhusu mkakati wake wa kuwekeza na kutanguliza zaidi maslahi ya wateja wake hususani katika mipango yake muhimu ikiwemo ile ya uvumbuzi na utoaji wa huduma kwa wateja.
Akizungumza kuhusiana na mkakati huo jijini Dar es Salaam mwishoni nwa wiki, Ofisa Mtandaji Mkuu wa Benki hiyo Bw Jaffari Matundu alisisitiza kuwa benki hiyo imejizatiti kuhakikisha kwamba wateja wake wananufaika zaidi na ukuaji wa technolojia katika utoaji wa huduma za kibenki.
"Lengo ni kuhakikisha kwamba benki ya Exim tunatumia vyema huu ukuaji wa kidigitali katika utoaji wa huduma za kibenki kwa wateja wetu…lengo ni kuona wanaridhishwa na huduma zetu na wanazifurahia. Tunaamini kwamba furaha na ukuaji wao ndio biashara yetu,'' alisema.
Aliongeza kuwa agenda ya uvumbuzi imebaki kuwa kipaumbele cha benki hiyo katika kuelekea kwenye lengo lake la msingi ambalo ni kuifanya benki hiyo kuwa ya kidigitali zaidi huku kipaumbele kikibaki kuwa ni 'mteja kwanza'.
Katika kabiliana na changamoto ya COVID 19 benki hiyo mapema mwaka jana ilizindua kampeni ya "Maliza Kirahisi Kidigitali' iliyodumu katika kipindi cha mwaka mmoja ikilenga kubadilisha tabia ya wateja na kuongeza kasi ya mabadiliko yanayoendelea ya nchi kutoka katika kutumia pesa taslimu kwenda malipo ya dijiti.
"Kampeni hiyo pia inakwenda sambamba na kuunga mkono mkakati wa Serikali wa kuhamasisha matumizi ya kidigitali katika kufanya miamala uchumi pamoja na kuhakikisha wateja wetu wanahudumiwa bila kwenda kwenye matawi" aliongezea.
Ili kurahisisha zaidi miamala na kuifanya bora zaidi na rahisi kwa wateja, benki ina chaguzi kadhaa za huduma kupitia simu na kidigitali ambazo wateja wanaweza kuzitumia kupata huduma na kufanya miamala muda wowowte katika siku saba za wiki. Katika kuhakikisha kwamba huduma za benki hiyo zinakuwa jumuishi, huduma ya USSD ndio ilihusika katika kuipamba kampeni hiyo.
''Kila mwingiliano na mteja ni nafasi kwetu kuwaelewa vizuri wateja wetu na namna ya kuwahudimia kulingana na mahitaji yao. Tunapoendelea kupanua huduma zetu, tunaweza kuona jinsi kila huduma inatimiza mahitaji ya watumiaji. Ni suala la kuendelea kujifunza na uvumbuzi. ’’
"Zaidi, kusikiliza kwa karibu maoni ya wateja hutusaidia kupata mrejesho unaotuwezesha kufanya maboresho na uvumbuzi ili kuimarisha huduma tunazowapatia. Lengo ni kufanya maisha yao yawe rahisi. Tunazingatia urahisi wa matumizi, na kufanya huduma zetu kuwa thabiti, salama, na haraka.'' alisema.
Ofisa Mtandaji Mkuu wa Benki ya Exim Bw Jaffari Matundu
By Mpekuzi
Post a Comment