Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amesema Jimbo la Hai limepata Mbunge hivi sasa, akiongeza aliyekuwepo kabla ya hapo alikuwa anazurura kila mahali.
Akiwa Bungeni Dodoma leo, Ndugai amesema, “Alikuwa haulizi maswali Bungeni, haeleweki. Lakini sasa Mbunge mnaye kabisa…”
Kauli yake imekuja baada ya Mbunge Saasisha Mafuwe kuhoji ni lini Serikali itatekeleza ahadi ya kumaliza mgogoro wa ardhi uliopo kati ya wananchi na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (KIA).
Mbunge huyo amesema mgogoro umekuwepo muda mrefu, na jambo hilo limesababisha wananchi kukosa maeneo ya malisho na kuishi kwa wasiwasi kwenye maeneo yao.
from Author
Post a Comment