Mambo 10 nilioyaona Mechi ya Yanga vs Azam Jana |Shamteeblog.



1: CLASSIC MATCH🙌 Kuna mechi makocha wanashinda. Kuna mechi Wachezaji wanashinda. PRINCE DUBE Ameshinda mechi yake kikatili sana. What A Player!

2: Kocha mpya wa Yanga alichofanikiwa kukiongeza kwenye timu ni ari tu. Kiufundi bado kidogo. Jambo jema kwake, amepata nafasi ya kuiona 'Yanga hii' kuelekea kuiunda Yanga yake ya msimu ujao. Kuna somo yeye na Uongozi wa Yanga wamelipata leo kutoka kwa Azam? Lipi hilo?

3: Timu zote zilikuwa bora katikati ya kiwanja lakini kilichoamua mechi, Azam mbele walikuwa na DUBE wakati Yanga mbele walikuwa na Sarpong na Yacouba. 'Quality' imewahukumu Yanga.

4: Credit kwa mwalimu George Lwandamina. Ule utatu katikati ya kiwanja (Muda/Bryson na Mbele kidogo Yahaya) umeklick vyema sana. Mapafu ya hawa watu yanawapa watu watatu wa juu kujiamini sana kwa kupokea huduma nzuri kwenye mikimbio yao

5: Nilienjoy sana vita ya katikati ya kiwanja. Mukoko was very Tough, Muda mbishi, Bryson mgumu..🙌 Kikaumana kweli kweli. Ikapigwa show moja ya kibabe sana

6: PRINCE DUBE🙌 WoW.. WHAT A PLAYER. Kwa 'viatu' vile vya Ninja, straika mwingine wa wasiwasi angenyongea.. Lakini Dube alionyesha CLASS yake. WoW🙌 Hana papara.. Bonge la Bao!

7: NINJA.. Yanga imepoteza mchezo katika siku ambayo alikuwa bora sana kiwanjani🙌 Timing yake kwenye kupokonya mpira ilikuwa ya viwanja sana. Kuna shida aliipitia kiasi kwa Dickson Job.. kivipi?

8: Kuanzia Dakika ya 70 Dickson Job alionyesha kuchechemea. Nafikiri bado ana jeraha mahala. Dube akawa anakimbia sana kwenye eneo lake. Ninja akalazimika kucheza kama namba 4 na 5 kwa wakati mmoja

8: Sarpong hakuna maajabu mengine ya kusubiri kutoka kwake. First touch yake ni mbovu sana. Hajiamini. Mara zote nguvu zinatangulia kabla ya akili

9: Mukoko Tonombe.. Captain Material👍 Jamaa anakaba, anatuliza timu na anaanzisha shambulizi. Mapafu yake yamejaa upepo wa kutosha.

10: Asante Mudathir kwa jasho lako👏 Asante Aggrey kwa uzoefu wako. Kibwana anaendelea kuimarika. Shikhalo ana la kujifunza kwa bao la Gwambina na hili la Dube

Nb: Tofauti ya Mwambusi na Mwarabu ni Kipara tu 😀

By Ali Kamwe


from Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post