MTOTO WA DARASA LA TATU AJIUA KWELI AKICHEZA NA WENZAKE NAMNA MTU ANAVYOJINYONGA |Shamteeblog.



Na Amiri Kilagalila, Njombe

Mwanafunzi wa darasa la tatu shule ya msingi Ikelu iliyopo Makambako mkoani Njombe, Claud Florence (9) amefariki dunia baada ya kujinyonga akiwa anacheza na wenzake.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe, Hamisi Issah amesema mwanafunzi huyo alikwenda shambani na wazazi wake na wadogo zake watatu akiwa huko alianza kucheza na wadogo zake na baadae kuchukua kikoi na kuanza kujaribisha namna mtu anavyojinyonga.

Amesema baada kufanya kitendo hicho katika mti pori uliopo hapo shambani matokeo yake alijikuta amening'inia kwenye mti huo huku wazazi wakiwa hawana taarifa yoyote wakiwa wanaendelea na kulima.

Amesema wazazi walipofika walifungua hicho kikoi na kumkuta mtoto wao akiwa taabani na kuchukua uamuzi wa kumpeleka hospitali na baadae kufariki dunia.

Amewataka wazazi kuwa makini na malezi ya watoto wao kwani malezi ya watoto ni pamoja na kuangalia aina ya michezo wanayocheza katika mazingira yanayofaa.

"Watoto hawa wamecheza michezo ya kupitiliza mpaka wamejaribisha kujinyonga na mwenzao mmoja kajiua kabisa", amesema Issah.






By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post