Na Amiri Kilagalila,Njombe
Wanachana wa Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA mkoani Njombe wametakiwa kuendelea kushirikiana ili kukijenga chama hicho hasa katika kipindi hiki ambacho wanajenga ofisi ya jimbo la makambako.
Akizungumza na wanachama wa chama hicho jimbo la Makambako mwenyekiti wa baraza la vijana (BAVICHA) Taifa JOHN PAMBALU amesema kuwa licha ya changamoto wanazokutana nazo kisiasa bado wapo imara na amewataka wanachama hao kuendelea kuwa na umoja na ushirikiano ili kukamilisha ujenzi wa ofisi kwa wakati.
Aidha mwenyekiti huyo ameonesha kufurahishwa na kitendo cha wanachama wa chadema jimbo la makambako kuanza ujenzi wa ofisi ya jimbo kwa kuchangishana fedha zao wenyewe bila kutegemea wafadhili na chama taifa na kueleza kuwa kitendo hicho ni cha uzalendo na itakuwa funzo kubwa kwa wanachama wengine nchini.
“Mmeipa changamoto wilaya nyingine nyingi zijifunze kutoka Makambako,na mnawajibu wale wanaosema Chadema hainaga ofisi,Chadema tuna ofisi mpaka za wilaya zaidi kama ya Makambako”alisema John Pambalu
Aliongeza kuwa “Tanzania hakuna Chama chocote cha siasa kuanzia CCM mpaka vyote vilivyobaki isipokuwa Chadema peke yake ambacho wanaweza wakajenga ofisi za Chama kwa nguvu ya wanachama bila hata ya Ruzuku”aliongeza Pambalu
Akizungumza kuhusiana na ujenzi wa ofisi hiyo ambayo inajengwa mtaa wa makatani(kiumba) kata ya lyamkena ,Katibu wa chadema jimbo la makambako ,DAUD TWEVE amesema kuwa wametenga kila siku ya jumamosi kukukatana na kufanya maendeleo ya ujenzi wa ofisi hiyo na kueleza kuwa lengo lao mpaka kufikia mwezi wa sita ofisi iwe imeezekwa.
“Lakini pia malengo yetu ni kwamba jingo letu hadi kufikia mwezi wa sita tuwe tumelifunika,ofisi hizi tunajenga kwaajili ya kizazi hiki na kinachokuja hata wanaccm wanafahamu majengo yao yale hawakujenga peke yao na sisi tunaamini ofisi hii itatumika na watu wote”alisema Daud Tweve
Nao baadhi ya wanachama wa chama hicho cha CHADEMA jimbo la makambako wamesema kuwa kukalika kwa ujenzi wa ofisi hizo kutaenda kuboresha zaidi utendaji kazi wa chama hicho na kuepukana na gharama ambazo zinatumika kwa sasa kulipa kodi ya pango kwenye ofisi ambazo wamepanga.
Zaidi ya milioni 50 zitatumika ili kukamilisha ujenzi wa ofisi hiyo ambayo mpaka sasa ipo hatua ya renta.
Jengo la ofisi Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema jimbo la Makambako linaloendelea kujengwa jimboni humo kwa nguvu za wananchi.
By Mpekuzi
Post a Comment