NJIKU AWATAKA WANAFUNZI KUWA WAZALENDO |Shamteeblog.

Afisa Tarafa Kata ya Ikungi mkoani Singida,  Yahaya Njiku , akihutubia kwa niaba ya mkuu wa wilaya hiyo Edward Mpogolo wakati akizungumza na Vijana Wanafunzi wa Katoliki Tanzania (TYCS) wahitimu wa Kidato cha Sita wa Shule ya Sekondari Ikungi mkoani Singida  katika sherehe ya kuagana na wanafunzi wenzao wa kidato cha 

5-1 iliyofanyika juzi wilayani humo.


Vijana Wanafunzi wa Katoliki Tanzania (TYCS)  wahitimu wa Kidato cha Sita wa Shule ya Sekondari Ikungi wakiwa wamejipanga tayari kuingia ukumbini katika sherehe ya kuagana na wanafunzi wenzao wa kidato cha 5-1 iliyofanyika juzi wilayani humo.
Walimu wakiwa kwenye sherehe hiyo.
Wazazi wakiwa kwenye sherehe hiyo.
Vijana Wanafunzi wa Katoliki Tanzania (TYCS)  wahitimu wa Kidato cha Sita wa Shule ya Sekondari Ikungi wakiwa kwenye sherehe hiyo.
Afisa Elimu Kata ya Ikungi, Mghenyi Nkuwi, akizungumza katika hafla hiyo.
Vyeti vikitolewa.
Vyeti vikitolewa.
Wazazi wakiwa kwenye sherehe hiyo.
Picha ya pamoja na mgeni rasmi.
Mgeni rasmi akikabidhiwa keki..
Mshereheshaji wa sherehe hiyo (MC) akiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi na walimu.



Na Dotto Mwaibale, Singida.


AFISA Tarafa Kata ya Ikungi mkoani hapa Yahaya Njiku amewataka vijana wanafunzi wa Katoliki Tanzania (TYCS) waliohitimu kidato cha sita katika Shule ya Sekondari ya Ikungi kuwa wazalendo wa nchi yetu.

Njiku ambaye alikuwa mgeni rasmi kwa niaba ya mkuu wa wilaya hiyo Edward Mpogolo aliyasema hayo wakati akizungumza na wanafunzi hao katika sherehe ya kuagana na wanafunzi wenzao wa kidato cha 5-1 iliyofanyika juzi wilayani humo.

"Mnapaswa kuwa wazalendo na uzalendo unatafusiri nyingi kwanza unapaswa kuipenda nchi yetu kuifahamu  kuithamini na kuitunza." alisema Njiku.

Alisema wakiwa kama vijana wanaohitimu kidato cha sita na wale ambao wanaendelea na masomo ni lazima kwanza wawe wazalendo.

Alisema sisi tupo katika Taifa la Tanzania hatuna lingine zaidi ya Tanzania hivyo tunapaswa kulitunza na kulitetea popote pale duniani.  

Njiku aliwaambia vijana hao kuwa uzalendo unatakiwa kuuanza wakiwa na umri mdogo na kuwa hawawezi kuwa wazalendo pasipo kulielewa taifa lao kuanzia historia yake, misingi na jinsi lilivyopatikana.

"Niwaombe ninyi wahitimu na nyie mnaoendelea na masomo ni lazima mfahamu historia ya taifa letu kwani leo hii mpo hapa mna furaha kwa kucheza muziki, michezo mbalimbali na kubadilishana mawazo kuna watu waliteseka kuliangaikia taifa letu akiwepo Baba wa Taifa Hayati Julius Kambarage Nyerere na wenzake.

Alisema ni muhimu kwa vijana hao kusoma masomo ya uraia ili waweze kulielewa taifa lao kwani wakilielewa wataweza kulitetea.

Katika hatua nyingine Njiku aliwataka vijana hao kuwa mabalozi wa kuhamasisha amani hapa nchini na kuwaombea viongozi wetu hasa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye aliapishwa hivi karibuni kuongoza nchi baada ya aliyekuwa Rais wetu Dkt.John Magufuli kufariki.

Aliwataka wahitimu hao kuendelea kumuomba Mungu ili waweze kuendelea na masomo yao ya  elimu ya juu kwani kumaliza kidato cha 5-6 sio mwisho wa kusoma.

"Nyinyi wanafunzi mnakila sababu ya kuendelea na masomo kwani Serikali  kupitia Rais wetu Mama Samia Suluhu imeweka mazingira bora ya kusoma kwa kutoa elimu bure." alisema Njiku. 

Aidha Njiku aliwaambia wahitimu hao kuwa nidhamu na uwajibikaji ni jambo jema litakaloweza kuwafanya waishi vizuri wakiwa shuleni, nyumbani na jamii na bila kuacha kumuomba Mungu ambaye siku zote hawezi kumuacha mtu amuombaye.

Njiku aliwataka vijana hao kuto jiingiza katika vitendo visivyo na maadili badala yake watumie muda wao kwa kujisomea na kuendeleza vipaji vyao vya michezo walivyonavyo na kuwapa heshima wazazi wao wanao wasomesha kwa kufanya vizuri mitihani yao.

Wahitimu hao 19 katika risala yao kwa mgeni rasmi walitaja baadhi ya mafanikio waliyopata wakiwa shuleni ni kushiriki katika kuchangia ujenzi wa parokia ya mtakatifu Rita wa Kashia wilayani humo.



By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post