RAIS SAMIA AKERWA MJADALA WA WABUNGE KUMLINGANISHA NA MAGUFULI |Shamteeblog.


Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesikitishwa na mijadala inayoendelea bungeni ya kumlinganisha na mtangulizi wake, hayati John Magufuli.

Mjadala wenyewe ambao umeonekana kumkera Rais Samia Suluhu Hassan wa ni miongoni mwa wabunge wa chama kinachoongoza dola, CCM. Wabunge ambao wamegawanyika katika makundi mawili, wanaotetea rekodi ya rais aliyepita John Magufuli na ambao wanaoonekana kukosoa baadhi ya mambo ya utawala huo.

Akizungumza Jumapili Aprili 18, 2021 katika kongamano la viongozi wa dini, Samia amesema yeye na Magufuli ni kitu kimoja na anaendeleza kazi iliyofanywa na mtangukizi wake huyo aliyefariki dunia Machi 17, 2021 kwa ugonjwa wa moyo.

''Inasikitisha sana kuona kwamba watu wanapiga ngoma mitandaoni, lakini ngoma ile inachezwa bungeni, kwa kulinganisha watu na sio kulinganisha ajenda za kitaifa, ajenda ya kitaifa ni moja, mnalinganisha Magufuli na Samia hawa watu ni kitu kimoja''.

''Awamu ya sita haikutokana na uchaguzi, haikutokana na chama kingine cha siasa, imetoka ndani ya chama cha Mapinduzi, imetokana na uongozi uliokuwepo wa awamu ya tano.'' Alisema Rais Samia.


''Awamu ni maneno tu , lakini mambo ni yaleyale.



By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post