SATF yataoa rai kwa Bodi ya Mikopo Elimu ya Juu (HESLB) kuongeza wigo Utoaji Mikopo |Shamteeblog.

Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Social Action Trust Fund (SATF) Mariam Mwaffisi ametoa rai kwa bodi ya mikopo ya Elimu ya Juu nchini kuwa iangalie uwezekano wa kuwapatia mikopo wanafunzi wanaochaguliwa na serikali kujiunga na vyuo vya kati. 

 Mwafisi aliyalibainishwa haya mapema wiki hii jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza katika warsha iliyoandaliwa na Taasisi ya Social Action Trust Fund (SATF) iliyowakutanisha wanafunzi wanaoishi katika mazingira magumu wanaofadhiliwa na SATF na ambao wamefanya vizuri katika mitihani yao ya kidato cha sita mwaka 2020.

 “HESLB inalojukumu la msingi la kuhakikisha wanafunzi wanaotoka katika mazingira magumu kama hawa ambao baadhi yao ndoto zao ni kwenda kujiendeleza katika vyuo vya kati wanaweza kupata elimu na kufikia malengo yao” Alisema Mwafisi. 

 Akijibu rai ya Mwenyekiti wa Bodi ya SATF, Ofisa Mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Nicolaus Kasamia amesema  Bodi ya Mikopo ya elimu ya Juu nchini (HESLB) inaendelea na mchakato ili kuhakikisha wanafunzi wanaosoma vyuo vya kati waweze kupata mkopo kwa kuwa ngazi hiyo ni mojawapo ya eneo lenye kuzalisha wataalam wengi.

 Aliongeza kuwa, wameonelea wao pia kufanya hivyo kwasababu wameona kuna kozi hususani za udaktari na injinia zinatolewa kwa gharama kubwa katika vyuo hivyo, ambapo inasababisha wanafunzi kushindwa kusoma.

 Bw. Kasamia alisema kuwa mwaka jana walipeleka ombi lao wizarani lakini lilikataliwa, hivyo kwa mwaka huu wanatarajia  kupeleka tena ili kuwasaidia wanafunzi wanaosoma katika vyuo hivyo. 

 Awali Mwenyekiti wa bodi ya SATF, Mariam Mwaffissi aliwataka wanafunzi hao kutokubweteka bali waangalie kile kilichowapeleka shule.  Alisema kila mmoja ana ndoto zake hivyo kwenda chuo wasijione wamefika, wapambane ili waweze kufikia ndoto zao. 

 “Msibweteke kwa kuwa mmefika chuo, muangalie kile kilichowapeleka na kuhakikisha mnafikia ndoto zenu. Tuache mkumbo hao wengine wana mambo yao. Na zawadi mtakazopewa ziwe chachu katika kutekeleza masomo yenu msibweteke,”.

 Hata hivyo alitoa wito kwa bodi ya mikopo iwasaidie wale waliopata mkopo kutoka kundi hili walau usiwe chini ya asilimia 90 kwa kuwa hawana ndugu wa kuwasaidia katika masomo yao.

 Kuhusu mradi wa SATF alisema lengo lake ni kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu kupata elimu, na ujuzi wa kuweza kuajiriwa ama kujiajiri ambapo tangu mwaka 2015  mpaka 2019 wametoa zawadi kwa washiriki 160 waliofanya vizuri kwenye mitihani yao.

Alisema katika warsha hiyo imewakutanisha wanafunzi 38 kati ya 43 ambao wanawafadhiri kimasomo na wamefaulu kwenda vyuo vikuu pamoja na kuwapa zawadi ya laptop na mabegi. 

 “Kupitia warsha hii, wanafunzi hawa tumewaleta pamoja na kuwajengea uwezo wa maisha ya vyuoni ambapo itawasaidia kuepuka changamoto mbalimbali watakazokutana nazo,” alisema. 

 Zuhura Chagile, mwanafunzi kutoka chuo Kikuu cha UDOM, aliwashukuru SATF kwa msaada huo, ambapo alisema atahakikisha anafanya vizuri ili naye baadaye aweze kuwasaidia wengine.

 

  Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Social Action Trust Fund (SATF) Mariam Mwaffisi akizungumza katika warsha iliyoandaliwa na (SATF) kwa kuwakutanisha wanafunzi wanaoishi katika mazingira magumu wanaofadhiliwa na SATF na ambao wamefanya vizuri katika mitihani yao ya kidato cha sita mwaka 2020.
 Ofisa Mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) Nicolaus Kasamia akizungumza  wakati wa warsha hiyo
  Baadhi ya wanafunzi wanaofadhiriwa kimasomo na SATF na ambao wamefaulu kwenda vyuo vikuu mwaka huu wakifurahia zawadi ya laptop na mabegi walizotunukiwa katika warsha hiyo. 
 Mwanafunzi kutoka chuo Kikuu cha UDOM Zuhura Chagile, aliwashukuru SATF kwa msaada wa laptop na mabegi kwaniaba ya wanafunzi wenzake
Viongozi wa SATF wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi 43 wanaofadhiliwa na shirika hilo na ambao wamefanya vizuri katika mitihani yao ya kidato cha sita mwaka 2020.

 



By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post