Charles James, Michuzi TV
KATIKA kuhakikisha mitazamo ya vijana kuhusu mazingira inakua chanya, Shirika lisilo la kiserikali la Raleigh Tanzania wamekuja na mradi wa "Vijana na mabadiliko chanya kitabia juu ya usafi" lengo likiwa kupambana na magonjwa yanayosababishwa na uchafu wa mazingira.
Akizungumzia jijini Dodoma Mratibu wa mradi huo, Agustino Dickson amesema mradi huo utatoa semina kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Dodoma huku ikitekelezwa katika Mikoa minne ambayo ni Iringa, Dar es Salaam, Dodoma na Morogoro ambapo utahusisha vijana takribani 48,000 kutoka mikoa hiyo.
Amesema mradi huo umelenga kuleta mabadiliko chanya juu ya utunzaji wa mazingira kwa vijana ambapo utahusisha pia vijana kutoa mafunzo kwa vijana wenzao.
" Leo tumeanza kufanya usafi katika Soko la Mavunde hapa Chang'ombe na tutaendelea na maeneo mengine, tunaamini vijana wakipata mafunzo juu ya utunzaji wa mazingira tutakua tumepiga hatua kubwa sana kwani hili ndilo kundi kubwa kwa sasa.
Pamoja na kutoa mafunzo haya lakini pia tumekua tukishirikiana katika kufanya usafi maeneo mbalimbali na kutoa msaada wa vifaa vya usafi ikiwemo vihifadhia taka ambapo maeneo waliyofikia ni pamoja na Soko hilo la Mavunde na Shule ya Sekondari Dodoma," Amesema Dickson.
By Mpekuzi
Post a Comment