Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkta.Damas Ndumbaro ( katikati) akiwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Mary Masanja wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt.Allan Kijazi mara baada ya kutembelea Shamba la kutunzia Wanyamapori yatima na waliojeruhiwa la Makoa lililopo wilayani Hai mkoani Kilimanjaro ambapo Wizara imetoa siku saba kwa Uongozi wa mkoa kurekebisha kasoro za mikataba ya shamba hilo walioingia na Mwekezaji
Mwanzilishi wa Shamba la kutunzia Wanyamapori Yatima na waliojeruhiwa la Makoa, Elizabeth Stigmaller akitoa maelezo kwa Viongozi wakuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii wakiwa na Mwenyeji wao Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Anna Mghwira walipotembelea leo shamba hilo na kujionea wanyamapori mbalimbali wanaolelewa ndani ya shamba hilo mkoani hapo
Mhudumu wa shamba la kutunzia Wanyamapori Yatima na waliojeruhiwa la Makoa, Jeremia Nyalale akiwamwagia maji tembo ili kupoza kiwango cha joto katika miili yao.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkta.Damas Ndumbaro ( katikati) akiwa na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Anna Mghwira pamoja na Mbunge wa Hai, Saashisha Mafuwe ( watatu kushoto) wakimsikiliza Katibu Tawala wa wilaya ya Hai, Upendo Wella kabla ya kuanza kutembelea Shamba la kutunzia Wanyamapori yatima na waliojeruhiwa la Makoa lililopo wilayani Hai mkoani Kilimanjaro ambapo Wizara imetoa siku saba kwa Uongozi wa mkoa kurekebisha kasoro za mikataba ya shamba hilo walioingia na Mwekezaji. Mbele ni Mwanzilishi wa Shamba la kutunzia Wanyamapori Yatima na waliojeruhiwa la Makoa, Elizabeth Stigmaller
Mwanzilishi wa Shamba la kutunzia Wanyamapori Yatima na waliojeruhiwa la Makoa, Elizabeth Stigmaller (wa kwanza kulia) akitoa maelezo kwa Viongozi wakuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii akiwemo Waziri wa Wizara hiyo,Dkt,Damas Ndumbaro pamoja na Naibu Waziri wa wizara hiyo,Mhe, Mary Masanja ( wa kwanza kulia) wakiwa na Mwenyeji wao Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Anna Mghwira (mbele) walipotembelea leo shamba hilo na kujionea wanyamapori mbalimbali wanaolelewa ndani ya shamba hilo mkoani hapo
Mhudumu wa shamba la kutunzia Wanyamapori Yatima na waliojeruhiwa la Makoa, Jeremia Nyalale akiwa naye mtoto yatima tembo akimfuata wakati Viongozi wakuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii akiwemo Waziri wa Wizara hiyo,Dkt,Damas Ndumbaro pamoja na Naibu Waziri wa wizara hiyo,Mhe, Mary Masanja wakiwa na Mwenyeji wao Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Anna Mghwira walipotembelea leo shamba hilo na kujionea wanyamapori mbalimbali wanaolelewa ndani ya shamba hilo lililopo wilayani Hai mkoani Kilimanjaro
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkta.Damas Ndumbaro ( wa pili kushoto) akiwa na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Anna Mghwira 9 watatu kushoto) wakiwa na viongozi mbalimbali wakiangalia Wanyamapori yatima na waliojeruhiwa katika shamba la Makoa lililopo wilayani Hai mkoani Kilimanjaro . Wa kwanza kushoto Mwanzilishi wa Shamba la kutunzia Wanyamapori Yatima na waliojeruhiwa la Makoa, Elizabeth Stigmaller
(PICHA ZOTE NA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
**************************************
WIZARA ya Maliasili na Utalii imetoa muda wa siku saba kwa uongozi wa mkoa wa Killimanjaro kuhakikisha unarekebisha kasoro zilizo kwenye mikataba ya shamba la kutunzia wanyamapori yatima la Makoa kabla ya kupewa kibali cha kuleta Simba kutoka nje ya nchi kwa ajili ya matunzo.
Akizungunza mara baada ya kutembelea shamba la Wanyamapori la Makoa , Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro amesema kuwa shamba hilo linapokea wanyamapori yatima na majeruhi kutoka kwenye hifadhi zote hapa nchini.
Amesema kutokana na umuhimu wa shamba hilo, ipo haja ya Serikali ya Mkoa kusaidia Chama cha Ushirika cha Urudu Makoa ili kiweze kufahamu namna sahihi ya kuingia mikataba yenye tija kwa Taifa.
“Nimetoa siku saba kwa viongozi wa Mkoa kuhakikisha wanakisaidia Chama cha Ushirika cha Uduru Makoa ili waweze kurekebisha kasoro zilizojitokeza kwenye mikataba ya uwekezaji pia wafahamu, ukomo wa mikataba na nani wanaingia nae mikataba hiyo na manufaa yake kwa vyama vya ushirika na Taifa kwa ujumla,” Amesisitiza Dkt. Ndumbaro.
Aidha, amesema ziara yake imelenga kutazama bustani hiyo inayotunza wanyamapori waliojeruhiwa au yatima ambao hutunzwa hadi na baadaye kurudishwa kwenye hifadhi pindi wanapokuwa au kurejea katika hali zao za kawaida.
Dkt. Ndumbaro amesema kuwa Wizara imejiridhisha pasipo shaka malezi na mazingira ya utunzaji wa wanyamapori hao yanaridhisha licha yakuwa bado kuna ukakasi katika mikataba waliyoingia.
” Mkataba walioingia kati ya Makoa na Mwekezaji huyo haijafuata misingi ya kisheria na leseni iliyotolewa imetolewa kwa mtu binafsi ambaye si muhusika wa shamba hilo, hivyo tumewaagiza Mkoa kukamilisha kasoro hizo mara moja, wakikamilisha taratibu zote walete maombi yao yakuleta wanyamapori kutoka nje ya nchi tutayashughulikia, “amesema Dkt. Ndumbaro.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghwira amesema kumekuwa na ukakasi wa kufahamu Mwekezaji halisi ni nani ili kuingia mkataba jambo ambalo baada ya Waziri kufika kila kitu kimekuwa wazi.
” Muda wa siku saba tuliopewa unajitosheleza maana kila kitu kipo ni kiasi cha kujipanga kulingana na Sheria na taratibu kwa mwongozo wa wataalamu wetu,” amesema
Naye mbunge wa jimbo hilo Mhe. Saashisha Mafuwe amesema ujio wa Waziri Ndumbaro umesaidia kufungua ukurasa mpya wa utendaji wa vyama vya ushirika vianze kuingia mikataba itakayoleta mabadiliko na faida kwa Taifa.
“Ombi langu kwa Mawaziri wengine kufika jimboni hapa kwani upo umuhimu mkubwa wa Serikali kutupia jicho la pekee hasa katika mikataba ya vyama vya ushirika,” amesema Mhe. Saashisha
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika Uduru Makoa,Saeli Mafuwe amesema wamepokea maelekezo na maagizo ya wizara husika na watayafanyia kazi kwa mujibu wa taratibu, kanuni na sheria.
” Mkataba wetu unakataza Mwekezaji kumpangisha Mwekezaji mwingine, na hapa ndicho kilichotokea, tutakaa na timu ya wataalamu kutoka wilayani na mkoani, ili kuona namna ya kutatua matatizo haya,”
Katika ziara hiyo walikuwepo Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja, Katibu Mkuu, Dkt. Allan Kijazi na Wataalamu mbali mbali kutoka Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii ambazo ni TAWIRI, TAWA na TANAPABy Mpekuzi
Post a Comment