VIONGOZI WA SERIKALI WAPIKWE NA TAASISI YA UONGOZI- WAZIRI MCHENGERWA |Shamteeblog.

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mohamed Mchengerwa amezitaka  wizara, idara na taasisi za Serikali kuhakikisha zinapitisha viongozi wake katika mafunzo yanayoandaliwa na kutolewa na Taasisi ya UONGOZI.

Mchengerwa ameyasema hayo leo Aprili 19,221  wakati wa ziara yake katika taasisi hiyo ambapo amesema taasisi zote hapa nchini ambazo zina watumishi wa umma wajipange, watenge bajeti zao kuhakikisha kwamba wanapita kwenye taasisi hii ili tuweze kupikana zaidi.

"Na wale ambao tunaamini wanaweza kutusaidia, tuwatumie. Tunao Wakuu wa Mikoa ambao wana uzoefu zaidi, waiteni na kuwatumia ili kuendelea kutoa elimu. Wakuu wa Mikoa na Wilaya ambao ni vijana na pengine wanadhani wao wakishateuliwa ndiyo wameshamaliza, kwamba hakuna mamlaka ya kuwachunguza na kuwafuatilia, ni lazima tuzingatie sana,” amesema Waziri huyo.

Aidha, Waziri Mchengerwa ametoa  msisitizo kuhusu suala la utendaji kazi kwa wizara, idara na taasisi zote za serikali; ikiwemo kuhakikisha kwamba stahiki za watumishi wa umma zinapatikana kwa wakati na kwa mujibu wa sheria, kuhakikisha  watumishi wanaokaimu nafasi mbalimbali kwa muda mrefu waweze kuthibitishwa katika nafasi hizo.

Endapo wana sifa zinazostahili, na kuhakikisha maadili na taratibu za utumishi wa umma zinazingatiwa ili kuleta ufanisi katika kazi na huduma zitolewazo kwa wananchi.

Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya UONGOZI Kadari Singo, akimkaribisha Waziri Mchengerwa kuongea na watumishi wa Taasisi hiyo.
Waziri Mchengerwa (Kushoto) akisikiliza wasilisho juu ya programu za Taasisi ya UONGOZI, pembeni yake ni Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya UONGOZI, Bw. Kadari Singo.
Waziri Mohamed Mchengerwa akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa Taasisi ya UONGOZI.
 


By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post