WAENDESHA BODABODA WANATAKIWA KUJITUMA KATIKA KULETA MAENDELEO - MWENISONGOLE |Shamteeblog.


Mwenyekiti wa Taasisi ya Maendeleo ya Pikipiki Edward Mwenisongole akizungumza na katika kikao ikiwa ni pamoja na kuunga mkono ya kufanya kazi kwa bidii Kama Rais Samia Hassan Suluhu alivyohutubia Bunge hivi karibuni.


Na Chalila Kibuda, Michuzi Tv 

VIJANA Nchini wametakiwa kuhakikisha wanachapa kazi kwa kutumia fursa zilizopo kwa madai kuwa kufanya hivyo kutakuwa ni kuunga mkono juhudi za Rais Suluhu Hassan ambaye amesema kuwa 'Kazi Iendelee'

Wito wa vijana kujituma umetolewa Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti kutoka Taasisi ya Maendeleo ya Pikipiki Jijini hapa Edward Mwenisongole wakati wa kikao na wajumbe  wa taasisi hiyo pamoja na wadau mbalimbali wa Maendeleo.

"Leo tulikutana kujadili mambo mbalimbali lakini kubwa likiwa ni lile la vijana kutumia fursa zilizopo kwa kufanya kazi na kujiongezea kipato kikubwa katika kumuunga mkono Rais Mama Yetu," alisema Mwenisongole, na kuongeza;

"Tunaamini vijana wanapojishughulisha kwa kutumia fursa na kwa kujua kwamba wanatakiwa kuitumikia Nchi yao ndilo jambo la msingi zaidi lakini pia wafanye kazi kwa bidii na hiyo ndiyo itakuwa njia pekee ya kumuenzi Hayati Rais John Pombe Magufuli kwa kauli yake ya hapa kazi tu,"alisema.

Meneja Miradi kutoka katika Taasisi hiyo Charles Sabiniani maalufu kama (Lowasa), alisema anaipongeza sana hotuba ya Rais Mama Samia Suluhu kwani pamoja na mambo mengine lakini anaona ni kwa jinsi gani vijana wataendelea kunufaika na uongozi wake kama walivyokuwa wananufaika wakati wa uongozi wa Hayati Magufuli.

Lowasa anbaye ni mjasiliamali na Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) anasema "mimi nikiwa kijana sina wasiwasi kwamba vijana tunaenda kunufaika na raslimali za Nchi yetu ikilinganishwa na Hotuba ya Rais Samia Hassan ya hivi karibuni bungeni kwa watanzania wote,"alisema.

Aidha alitumia nafasi hiyo kuwaomba vijana kuendelea kujituma kwa kufanya kazi kwa bidii na kusema kuwa kufanya hivyo kutakuwa ni kumuunga mkono Mwanamke wa kwanza Rais Samia.

"Pia kuunga mkono kauli yake ya kazi iendelee lakini mimi nikiwa Meneja miradi ninayo malengo makubwa juu ya vijana wenzangu katika kuhakikisha tunaendelea kubuni miradi lengo likiwa ni kuchochea uchumi wa Nchi," alisema Lowasa. 

Alisema ni wakati muhafaka kwa vijana Tanzania Bara na Visiwani na hasa wale madereva bodaboda na Bajaji kuendelea kujituma na kufanya kazi kwa bidii huku wakiendelea kutunza Amani ya Nchi na kuacha kushiriki kwenye vitendo vinavyoweza kuashiria uvunjivu wa Amani.

Hata hivyo Meneja huyo alisema kuwa ametembelea maeneo mbalimbali ya Jiji hili na kujionea vijana wanavyojituma kwa kufanya kazi katika kuendelea kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan kwa kauli yake ya 'Kazi iendelee.'



By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post