WAFANYAKAZI WA PROGRAMU YA KUMALIZA MALARIA ZANZIBAR WASHIRIKIANA NA KAMATI ZA USAFI ZA SHEHIA KUFANYA USAFI KIKWAJUNI BONDENI MJINI ZANZIBAR |Shamteeblog.


Na Ramadhani Ali – Maelezo 


Programu ya kumaliza Malaria Zanzibar wakishirikiana na Kamati za Shehia za kuimarisha usafi na kuondosha mazalia ya mbu wamefanya usafi katika shehia za Kikwajuni bondeni ikiwa ni moja ya maadhimisho ya siku ya Malaria Afrika.

Maadhimisho ya siku ya Malaria Afrika ambayo hufanyika kila mwaka ifikapo tarehe 25 Aprili, kwa Zanzibar mwaka huu yataadhimishwa tarehe 22 Aprili katika Ukumbi wa Idriss Abdulwakil Kikwajuni.

Akizungumza na Waandishi wa habari wakati wa zoezi la usafi, Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Dk. Fadhil Muhd Abdalla alisema kuondosha uchafu na mazalia ya mbu ni muhimu katika kumalliza kabisa maradhi hayo ifikapo mwaka 2023.

Dk. Fadhil alisema kiwango cha Malaria Zanzibar sio kibaya lakini baadhi ya maeneo hasa ya Mkoa Mjini Magharibi yanaonekana kuongezeka kwa maradhi hayo.

Hata hivyo alieleza kuwa agonjwa wengi wanaogundulika kuugua malaria wengi ni waliotoka nje ya Zanzibar ama Wazanzibari waliosafirki nje ya Zanzibar kwa shughuli zao mbali mbali.

Aliwashauri wananchi wanapoona dalili za kuugua malaria kwenda vituo vya afya kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi na kupatiwa matibabu ili kuwanusuru wananchi wengine kuambukizwa maradhi hayo.

Aidha aliwataka wananchi kuendelea kutumia vyandarua vilivyotiwa dawa, kuendeleza usafi katika maeneo yao na kuondosha mazalia ya mbu hasa katika kipindi hichi cha mvua za masika ili kujiepusha na Malaria na maradhi mengine.

Kaimu Meneja wa Programu ya kumaliza Malaria Zanzibar Dk. Faiza Bwanakheri Abass alisema wameamua kuunda Kamati za Shehia za kuimarisha usafi na kuondoa Malaria ikiwa ni moja ya njia ya kuihamasisha jamii kushiriki katika mapambano hayo.

Afisa uhamasishaji Programu ya kumaliza Malaria Zanzibar Dk. Mwinyi aliwataka wanchi wanaogundulika kuugua malaria waweke anuani zao kamili kwani wanakuwa wanafanya ufuatiliaji kwa kila mgonjwa ili kujua maendeleo yake na afya za majirani zake.

Baadhi ya wajumbe wa kamati za usafi za Shehia Wilaya ya Mjini wakishirikiana na Programu ya kumaliza Malaria Zanzibar wakifanya usafi kuondosha mazalio ya Mbu katika shehia za Kikwajuni bondeni ikiwa ni moja ya maadhimisho ya siku ya Malaria Afrika.

Mtaalamu wa Malaria sehemu ya Mbu Makame Ali Shehe akimuonyesha sehemu wanazopenda kukaa mbu Kaimu Meneja wa Programu ya kumaliza Malaria Zanzibar Dk. Faiza Bwanakheri Abass wakati wa usafi katika shehia za Kikwajuni bondeni.
Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Dk. Fadhil Mohd Abdalla akizungumza na wandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya siku ya Malaria Afrika ambayo hufanyika kila mwaka ifikapo tarehe 25 Aprili ambapo kwa Zanzibar yataadhimishwa kesho  Aprili 22 katika Ukumbi wa Idriss Abdulwakil Kikwajuni Mjini Zanzibar.Picha na Makame Mshenga.


By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post