Na Jusline Marco-Arusha
Mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji la Arusha Dkt.John Pima amewataka wanafunzi wa chuo cha uhasibu Arusha IAA kuwa na muelekeo wa kule wanapotaka kuelekea kwa kuweka bidii katika masomo yao na kuwa wabunifu.
Akifungua hafla ya IAA CAREERS DAY iliyofanyika chuoni hapo Dkt.Pima amekipongeza chuo hicho kwa kuendeleza hafla hiyo kwani wanafunzi wengi wamefanikiwa na kufika mbali kupitia careers day zilizopita hivyo ni matarajio yake mwaka huu wanafunzi wengi watakuwa na ubunifu mkubwa.
"Niwaombe sana wale wote ambao mnamipango yenu lazima muwe na ubunifu unaobebwa na uzoefu kutoka kwa watu wengine ndio utakao wawezesha kufika katika hatma yenu na kujua mnakwenda wapi."Alisema Dkt.Pima
Aidha alisema kuwa ili waweze kufikia mafanikio yao vipo vitu ambavyo vinawaongoza kuwa ni kusoma na kufanya kazi kwa bidii pamoja na kuweka mipango thabiti katika kuifikia hatma yao hivyo IAA CAREERS DAY iwasaidie kujua wapi wanapotakiwa kuwa.
Awali akizingumza katika hafla hiyo Gloria Kimburu Kaimu Mkuu wa Chuo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mafunzo alisema kuwa kutokana na mabadiliko katika soko la ajira chuo hicho kiliona umuhimu wa kuendelea kutumia IAA BUSSINES STATUP CENTER ili kuweza kuendelea kuwaandaa wanafunzi kujiajiri kupitia uvumbuzi,ubunifu na ujasiriamali ambapo wameweza kuwafikia baadhi ya wanafunzi na kuanza kuona matokeo.
Sambamba na hayo alisema kama chuo kwa mwaka huu wa masomo wameanzisha mtaala yenye kozi ambazo zinajikita kutoa ujuzi zaidi na kuwawezesha wanafunzi kuwa katika kazi muda mwingi zaidi ya masomo huku wakipata ujuzi zaidi ambapo tayari wameanza na mitaala miwili huku mwaka ujao wa masomo wanatarajia kuongeza mitaala itakayoelekeza kwenye aprentship lengo likiwa ni kuhakikisha wanafunzi wanakuwa na maarifa na ujuzi wa kutosha katika fani zao ili kuwawezesha kuweza kujitegemea na kushindana katika dunia ya sasa.
"Karne hii teknolojia imekuwa rasilimali muhimu kwa maendeleo na chanzo cha ushindani kwa sekta ya uzalishaji na huduma."alieleza Bk.Kimburu
Vilevile alisema katika dira mwaka 2025 serikali inasisitiza juu ya kuchochea na kukuza utamaduni wa sayansi na utamaduni wa uvumbuzi wa kiteknolojia katika jamii ambapo ni kazi ya setikali,taasisi za elimu na mashirika yasiyo ya kiserikali kuanzisha miongozo na programu za ufumbuzi,ukuzaji na uendelezaji wa ubunifu wa ndani na wavumbuzi nchini ili kuhimiza ubunifu katika jamii ya watanzania hususani kundi la vijana ambapo kama chuo wameanza na wataendelea kujikita katika hilo.
Kwa upande wake mshiriki wa careers day kwa mwaka 2021,Silas Ruben na mshindi wa kwanza katika mashindano hayo ambaye aliyekuwa akiwasilisha wazo la teknolojia ya kupima umeme kwa saa,siku na kuweka rekodi ya mwezi mzima ya matumizi ya kiwango cha umeme kilichotumika.
"Teknolojia hiyo inapima umeme bila ya kuchubuwa nyaya ambapo unaunganisha kwenye moja wapo kati ya hasi au chanya na kusoma kipimo chetu moja kwa moja kwenye vifaa vya kompyuta ambavyo vinaweza vikawa ni simu au kifaa chochote kile kinaweza kuwa na mtandao."Alisema Silas
Aliongeza kuwa mashindano hayo yamesaidia kuonyesha uwezo wa mtu alionao na kuuweka katika uhalisia na kuwafanya watu waweze kuona au kupata ufadhili utakao wawezesha kuendeleza vipaji vyao.
Sambamba na hayo mmoja wa washiriki wa mashindayo hayo ambayo yaliandaliwa na wanachuo katika chuo cha uhasibu Arusha,Emmanuel Mkenda alisema ili kuweza kukabiliana na changamoto ya ajira kama vijana wanapaswa kuwa wabunifu kwa kupambana na vipaji walivyonavyo kwa kuviendeleza na kuvifanyia kazi ili ziweze kutatua changamoto na kuwa kama sehemu ya ajira kwao kwa kutengeneza mazingira ambayo yataleta tija katika jamii na kuwanufaisha.
Akielezea kupitia kikundi chao cha Forest Fire Dictector wameanzisha kitu ambacho wakikifanyia kazi kitaleta manufaa katika jamii na kuwafanya watu kuweza kukitumia hatimaye kutatua changamoto zote ambazo zinawakuta watu katika jamii kipitia bidhaa hiyo.
Aliongeza kuwa kupitia kifaa hicho ambacho ni kiashiria moto,mtu au mamlaka husika inaweza kupata taarifa za awali za kuwepo na tatizo la moto ambazo zitamuwezesha mtu kudhibiti moto huo kwa haraka.
Naye waziri mkuu (IASO)katika serikali ya wanafunzi chuoni hapo,Steven Geofrey Lomo alieleza kuwa carrers day ji siku ambayo wamekuwa wakiifanya karibu kila mwaka wa masomo kwa ajili ya wanafunzi kuonyesha mambo ambayo hujifunza darasani na kuyaleta katika uhalisia.
"Imekuwa ni jukwaa ambalo linaweza kikuza kipaji cha mwanafunzi kwani tuna wanafunzi ambao ni washiriki wanaonyesha ubunifu wao na kuwaunganisha pamoja na waajiri hivyo tumealika wageni kutoka makampuni na taasisi mbalimbali kuja kuona ni kwa namna gani chuo chetu cha Uhasibu kinawapika na kinawakuza watu katika soko la ajira huko nje"Alisema Steven
Alieleza kuwa careers day ya mwaka huu ni tofauti naya mwaka uliopita kutokana na ubunifu waliouongeza kwa kuangalia talanta na vipaji mbalimbali vya wanafunzi kwani vipaji vya watu vimekuwa ni soko kubwa la kumuinua mtu na kuongeza kipato cha mtu mmoja mmoja na uchimi wa nchi.
Aliongeza kuwa chuo cha uhasibu kkmekuwa ni chuo ambacho hupika wanafunzi kupitia IAA BUSSINES STATAUP CENTER katika biashara mbalimbali ambazo huanzishwa kwa lengo la kuwakuza na kuwakutanisha na masoko ya nje.
Waziri Mkuu (IASO) Serikali ya wanafunzi chuoni hapo,Steven Geofrey Lomo akizungumza katika siku hiyo ya Careers ambayo ililenga kuibua vipaji na ubunifu kwa wanafunzi.
Silas Ruben mshindi wa kwanza katika shindano lililoendeshwa na wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Arusha katika siku ya Careers kwa mwaka 2021.
Mkurugenzi wa jiji la Arusha Dkt.John Pima akizungumza na wanafunzi wa chuo cha Uhasibu Arusha katika siku ya Careers Day wakati alipokuwa mgeni rasmi.
By Mpekuzi
Post a Comment