TAARIFA KWA UMMA
WITO WA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA JKT MUJIBU WA SHERIA MWAKA 2021
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), linawaita vijana waliohitimu elimu ya sekondari kidato cha sita kwa mwaka 2021, kutoka shule zote za Tanzania Bara kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa mujibu wa Sheria.
Sanjari na wito huo, JKT limewapangia makambi watakayo kwenda kupatiwa mafunzo na wanatakiwa kuripoti makambini kuanzia tarehe 01 hadi 10 June 2021.
Vijana walioitwa wamepangwa katika kambi za JKT Rwamkoma - Mara, JKT Msange - Tabora, JKT Ruvu - Pwani, JKT Mpwapwa, na Makutupora JKT Dodoma, JKT Mafinga - Iringa, JKT Mlale - Ruvuma, JKT Mgambo na JKT Maramba -Tanga, JKT Makuyuni - Arusha, JKT Bulombora, JKT Kanembwa, na JKT Mtabila - Kigoma, JKT Itaka - Songwe, JKT Luwa na JKT Milundikwa - Rukwa, JKT Nachingwea - Lindi na JKT Kibiti- Pwani na Oljoro JKT- Arusha.
Wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho (Physical disabilities) waripoti katika kambi ya Ruvu JKT iliyopo Mlandizi Mkoani Pwani ambayo ina miundombinu ya kuhudumia watu wa jamii hiyo.
JKT linawataka vijana hao kuripoti wakiwa na vifaa vifuatavyo.
- Bukta ya rangi ya ‘Dark Blue’ yenye mpira kiunoni (lastic), iliyo na mfuko mmoja nyuma, urefu unaoishia magotini, isiyo na zipu.
- T-shirt ya rangi ya kijani (Green Vest)
- Raba za michezo zenye rangi ya kijani au blue.
- Shuka mbili za kulalia zenye rangi ya blue bahari.
- Soksi ndefu za rangi nyeusi.
- Nguo za kuzuia baridi kwa waliopangiwa mikoa yenye baridi.
- Track suit ya rangi ya kijani au blue
- Nauli ya kwenda makambini na kurudi nyumbani.
Orodha kamili ya majina ya vijana walioitwa, Makambi ya JKT waliyopangiwa na maeneo yaliyopo inapatikana hapo chini.
BOFYA JINA LA KIKOSI HAPO CHINI KUANGALIA MAJINA YA VIJANA WA MUJIBU WA SHERIA 2021
Tafadhali bonyeza jina la kikosi kutafuta jina lako
Mkuu wa JKT Brigedia Jenerali Rajabu Mabele, Anawakaribisha vijana wote walioitwa ili waweze kujiunga na vijana wenzao katika kujifunza uzalendo, umoja wa kitaifa, stadi za kazi, stadi za maisha na utayari wa kulijenga na kulitumikia Taifa.
By Mpekuzi
Post a Comment