Licha ya uwepo wa janga la Virusi Corona ambalo bado limeendelea kuathiri shughuli za michezo mingi duniani kote kwa kukosa wahudhuriaji viwanjani (mashabiki) na hata mingine kuahirishwa.
Bondia wa UFC Conor McGregor ametajwa na Forbes kuingiza kiasi cha dola milioni 180 sawa na TZS Bilioni 417.4 kwa kipindi cha miezi 12.
McGregor ndiye kinara huku akifuatiwa nyota wawili wa mchezo wa mpira wa miguu duniani, Lionel Messi na Cristiano Ronaldo, na ikielezwa kuwa pesa yake nyingi imetokana na mauzo ya kinywaji chake cha Whiskey lakini dola milioni 22 aliingiza kutokana na pambano lake UFC 257 mwezi Januari.
Orodha (Top 10) kamili hii hapa.
1.Conor McGregor – $180M
2.Lionel Messi – $130M
3.Cristiano Ronaldo – $120M
4.Dak Prescott – $107.5M
5.LeBron James – $96.5 M
6.Neymar – $95M
7.Roger Federer – $90M
8.Lewis Hamilton – $82M
9.Tom Brady – $76M
10.Kevin Durant – $75M.
from Author
Post a Comment