Ditopile amuwashia moto mkali Zito Kabwe kampeni za Buhigwe |Shamteeblog.





TUMETUA! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya Timu ya wabunge watatu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mariam Ditopile, Aesh Hilaly na Santiel Kirumba kuwasili wilayani Buhigwe,Kigoma kushiriki kampeni za mgombea wa Chama cha Mapinduzi CCM, Kavejuru Felix.

Jimbo la Buhigwe limeingia kwenye kampeni baada ya aliyekua Mbunge wa Jimbo hilo, Dk Philip Mpango kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais baada ya aliyekua Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan kuapishwa kuwa Rais .

Akizungumza baada ya kutua wilayani hapo na kukutana na Katibu wa Wilaya wa CCM, pamoja na viongozi wengine katika kikao cha ndani sambamba na wafanyabiashara wadogo wa Buhigwe, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma, Mariam Ditopile amesema linapokuja suala la uchaguzi CCM haina shughuli ndogo huku akituma salamu kwa Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe akimtaka amtafutie mgombea wake kazi nyingine kwani Buhigwe ni jimbo la CCM.

Ditopile amesema wananchi wa Jimbo la Buhigwe wameona matunda ya kuichagua CCM katika uchaguzi mkuu uliopita na wamepata heshima ya kupata Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivyo kuwaomba wananchi wa Buhigwe kutofanya makosa Mei 16 na wamchague Kavejuru Felix.

“ Tunafahamu Zito Kabwe anapitapita mitaani kuwalaghai wananchi ili wamchague mgombea wake, lakini niwaambie wana Buhigwe heshima mliyopewa ya kutoa Makamu wa Rais ni kubwa sana na inabidi tumpe zawadi Rais Samia kwa kumletea Mbunge wa CCM ili ashirikiane na Makamu wa CCM na Mbunge wa CCM katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Buhigwe.

Huyo Zito Kabwe na chama chake wameshachokwa na watanzania, kazi yake ni kuwalaghai wananchi kwa ahadi zisizotimizika, niwasihi sana ndugu zangu wa Buhigwe maendeleo yenye kasi yataletwa tukiwa na Mbunge wa CCM ambaye atazungumza lugha moja na Makamu wa Rais Dk Mpango mtoto wa nyumbani na Rais Samia Suluhu Hassan, hawa wote wanatekeleza ilani ya CCM katika kuwaletea maendeleo watanzania,” Amesema Ditopile.


from Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post