Mbunge wa kuteuliwa Dkt. Bashiru Ally amempongeza Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai, kwa namna anavyoendesha shughuli za bunge hususani kwenye bajeti ya Wizara ya Kilimo.
Bashiru ambaye alikuwa anachangia kwa mara ya kwanza bungeni amesema kuwa Kilimo ndio inabeba hatma ya maisha ya watanzania na Spika Ndugai amesimama na wananchi kuhakikisha serikali kupitia bajeti ya Wizara ya Kilimo inatatua changamoto zinazokabili sekta hiyo.
Aidha kwa upande mwingine ametoa pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Makamu wake Dkt. Philip Mpango kwa namna ambavyo wameshika hatamu na kulivusha taifa katika kipindi kigumu lilichopitia.
from Author
Post a Comment