Washiriki pia walipewa elimu ya namna ya kupambanana ukatili wa kijinsia katika jamii inayowazunguka
Mkurugenzi Mtendaji wa Gender Action Tanzania(GATA) Neema Makando akimkabidhi zawadi aliyekuwa mshindi wa tatu Anette Dancan aliyekimbia kilometa 21 katika mbio za GBV PREVENTION MARATHON zilizofanyika mwishoni mwa wiki,Goba mkoani Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Gender Action Tanzania(GATA) Neema Makando (wa nne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa mbio za GBV PREVENTION MARATHON zilizofanyika mwishoni mwa wiki,Goba mkoani Dar es Salaam.
**
WASHIRIKI zaidi ya 200 wameshirki GBV Prevention Marathon kwa kukimbia mbio za kilometa 21, kilometa 10 pamoja na kilometa 5 huku ikielezwa sababu za kuandaliwa marathon hiyo ni kupinga ukatili wa kijinsia katika jamii ya Watanzania.
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari , Mkurugenzi Mtendaji wa Gender Action Tanzania(GATA) Neema Makando amesema wameamua kuandaa mbio hizo za Marathon kwa ajili ya kufikisha ujumbe kwa jamii ya Watanzania katika kupinga ukatili wa kijinsia pamoja na kutambua madhara ya ukatili huo.
"Tumekutana hapa leo kwenye mbio hizo za GBV Prevention Marathon kwa ajili ya kupeleka ujumbe wa kupinga masuala ya ukatili wa kijinsia , kwa hiyo kukimbia mbio hizi ni sehemu ya michezo, sehemu ya kujiburudisha , inaleta watu pamoja na kwetu hii ni nafasi ya kuzungumza masuala ya kujinsia, hatua za kuchukua, kukemea na kuzuia.
"Hivyo jamii itakuwa inajua kuhusu ukatili wa kijinsia, aina za ukatili na hatua za kuchukua ili kuukomesha, kwa hiyo wote leo tumekuwa mashuhuda wa mbio hizi ambapo washiriki wapato 200 wameshiriki kwa kukimbia umbali wa kilometa 21,kilometa 10 na kilometa tano.
"Tumetoa zawadi kwa washindi kuanzia mshindi wa kwanza hadi wa tatu katika mbio za kilometa 21, mbio za kilometa 10 na mbio za kilometa tano.Pamoja na kutoa zawadi ujumbe wetu kwa washiriki na wote walikuwepo kwenye marathon hiyo ni kuwaeleza ukatili wa kijinsia haukubaliki,"amesema.
Ametumia nafasi hiyo kuwashukuru wadau mbalimbali kwa kushiriki kwao kikamilifu katika kufanikisha marathon hiyo iliyoandaliwa kwa ajili ya kupinga ukatili wa kijinsia."Tunawashukuru wote ambao wametusaidia kufanikisha mbio hizi".Katika mbio hizo za marathon mshindi wa kwanza katika mbio za kilometa 21 amepata kitita cha Sh.200,000, mshindi wa pili Sh.150,000 na mshindi wa tatu amepata Sh.100,000
Kwa upande wa washiriki wa mbio hizo wametoa pongezi kwa GATA kwa kuandaa mbio hizo za Marathon kwa lengo la kupeleka ujumbe wa kupinga ukatili wa kijinsia na kwamba wanaamini jamii ikishiriki kikamilifu kuna uwezekano mkubwa ukatili huo ukakomeshwa.
Mshindi wa kwanza wa mbio za kilometa 21 Edson Mwakaluka ambaye ni Mwalim Msaidizi kutoka Klabu ya GRR , amesema wameshiriki marathon hiyo kwa lengo la kupinga ukatili wa kijinsia nchini."Nimekuwa mshindi wa kwanza katika mbio za kilometa 21, tunaunga mkono kampeni hii ya kuzuia unyanyasaji na ukatili wa na jamii, hivyo tushirikiane kukomesha hali hiyo".
By Mpekuzi
Post a Comment