Lulu Adaiwa Kuwa Kuwa Mjamzito |Shamteeblog.




 
JE, ni mwendelezo wa “kufyatua’ watoto kimyakimya kwa mastaa wa kike Bongo kama alivyoanzisha ‘shoo’ hiyo Jackline Wolper?Inawezekana!
Maana baada ya Wolper kujifungua mtoto hivi karibuni kwa kuwaspraiz watu, gumzo limehamia kwa staa mwingine Elizabeth Michael ‘Lulu’ ambaye anatajwa kuwa ndoa yake na Francis Shiza ‘Majizo’ imelipa.

Lulu na Majizo walifunga ndoa yao Februari 16, mwaka huu, jijini Dar es Salaam ambapo mara kadhaa Lulu amekuwa akiripotiwa kuwa ni mjamzito.

Hata hivyo, Majizo alipofanyiwa mahojiano na kituo kimoja cha habari hivi karibu na kuulizwa kuhusu mkewe kuwa mimba alisema: “Kama ipo itaonekana.

”Pengine kwa kuwa kujifungua siyo jambo la siri, mapema jana mtangazaji wa kituo kimoja cha Radio cha jijini Dar alimtaja laivu Lulu katika kipindi chake kuwa miongoni mwa wanawake maarufu Bongo waliojifungua hivi karibuni.


 
Tangu hapo, gumzo likahamia mitaani na kwenye mitandao ya kijamii, ambapo wengi walimpongeza staa huyo kwa hatua hiyo na baadhi kustaajabishwa na habari hizo kwa vile ni kama zimekuja ghafla.

“Kuhusu ujauzito taarifa nilikuwa nazo, lakini suala la kujifungua sijui,” rafiki wa karibu na Majizo aliliambia Amani kwa njia ya simu.

Pekua ya timu ya waandishi wenye weledi wa Amani ilipoingia kazini ilikosa chanzo cha uhakika cha kuthibitisha kwamba mwanamke huyo amejifungua mtoto gani na anaendeleaje baada ya kupitia hali hiyo nzuri katika maisha ya ndoa.


Mwandishi wetu alipojaribu kumtafuta Majizo kwa njia ya simu yake ya mkononi iliita bila kupokelewa huku simu ya Lulu ikionekana kuwa imezimwa.

Mtu wa karibu na familia ya Lulu alipoulizwa na mwandishi wetu kuhusu habari hizi njema alisema:“Sijasikia, hebu ngoja nipeleleze kwa mama yake halafu nitakujulisha.

”Hadi gazeti linakamilika kwa matayarisho, Amani halikuwa limejulishwa chochote kutoka kwa mtu huyo, lakini uvumi wa Lulu kujifungua ulikuwa ukienea mitaani kama moto wa kifuu.

Hivi karibuni Wolper alitumia staili ya usiri siyo kujifungua tu, bali hata kuonekana ana ujauzito miongoni mwa rafiki zake hadi habari kuwa amepata mtoto wa kiume ziliporipotiwa na AMANI kwa mara ya kwanza kisha baba wa mtoto ambaye ni Rich Mitindo naye akaanza kufunua mitandaoni kwa mara ya kwanza picha ya staa huyo alipokuwa mjamzito.


 
Amani linaamini huenda Lulu ambaye sasa anajiita ‘Mama G’ naye ameamua kupita njia hiyo ambayo Wolper aliipitia hadi pale timu ya Global ilipoibuka na kufichua kwa mara ya kwanza kuwa staa huyo amejifungua.

Kwa kuwa kujifungua siyo jambo la kashfa, ni suala la muda tu, kama hiki kinachosemwa ni cha kweli; kitabainika.Lakini yote kwa yote Amani liko pamoja na familia ya Lulu katika mema yote.


from Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post