Mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa umma na utawala bora Mhe Mohamed Mchengerwa akipokea zawadi maalum kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan kutoka kwa Mwenyekiti wa TAPSEA Zuhura Songambele Maganga kwa kuitambua kada hiyo muhimu na yenye mchango mkubwa.Mhe.Mchengerwa amefungua mkutano wa nane wa mwaka wa chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania {TAPSEA} jana katika ukumbi wa AICC jijini Arusha.Mkutano huo wa Mwaka umewakutanisha Makatibu Mahsusi zaidi ya 3000 kutoka mikoa mbalimbali nchini.Pichani kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.John Mongela.
Mwenyekiti wa TAPSEA Zuhura Songambele Maganga akimpokea Mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa umma na utawala bora Mhe Mohamed Mchengerwa alipokuwa akiwasili katika ukumbi wa AICC jijini Arusha leo kwa ajili kufungua mkutano wa chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania {TAPSEA} .Mkutano huo wa Mwaka umewakutanisha Makatibu zaidi ya 2000 kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini.
By Mpekuzi
Post a Comment