Mmiliki wa Kiwanda Bubu Akutwa na Stika za TRA |Shamteeblog.



Jeshi la Polisi Arusha linamshikilia mwanamke mmoja mkazi wa Sakina ambaye ni msimamizi wa kiwanda bubu kinachozalisha pombe kali na kumkuta akiwa na vitu mbalimbali ikiwemo stika 340 za TRA, chupa 483 za pombe kali, mtambo wa kutengenezea pombe pamoja na pipa lililojaa pombe kali lita 250


Taarifa hiyo imetolewa leo Mei 25, 2021, na Kamanda wa Polisi mkoani humo ACP Justine Masejo, na kuongeza kuwa mbali na vitu hivyo mwanamke huyo pia alikutwa na stika za kiusalama pakiti tatu, stika za pombe 700 na vifungashio vya chupa boksi 23.


"Upelelezi unaendelea na pindi utakapo kamilika jalada litapelekwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa hatua zaidi za kisheria, nitoe wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili kutokomeza kabisa uhalifu katika mkoa wetu na zoezi hili la ukamataji ni endelevu," amesema ACP Masejo.



from Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post