MUIGIZAJI MAARUFU WA FILAMU MZEE MSIRI AFARIKI DUNIA |Shamteeblog.

Muigizaji mkongwe anayefahamika katika kipindi cha Pete kama Mzee Msiri amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 62.

Gillie Owino kwa majina yake halisi alifariki dunia Ijumaa Aprili 30,2021 saa chache baada ya kukimbizwa hospitalini. 

Kulingana na taarifa kutoka kwa familia yake, Mzee Msiri aliangamizwa na ugonjwa wa saratani.

Mzee Msiri hakuonyesha dalili za kuwa mdhaifu hadi siku zake za mwisho ambazo pia alionekana akiwa studioni akiigiza.

 Familia ilisema kwamba marehemu amekuwa akipokea matibabu kwa miaka kadhaa lakini hali yake ilidorora ghafla Alhamisi Aprili 29 ambapo alikimbizwa hospitalini. 

Madaktari walijaribu kadri ya uwezo wao kuyaokoa maisha yake lakini Maulana alikuwa ashapanga mpango wake wa kumchukua.

 Mzee Msiri alikuwa mwandishi na mkurugenzi wa filamu hasa katika maeneo ya mkoa wa Pwani.

Mashabiki wake watamkosa sana hasa katika kipindi cha Pete ambacho hupeperushwa kwenye runinga ya Maisha Magic.

 Kando na kuwa muigizaji, Mzee Msiri pia alikuwa mhasibu mstaafu. Mzee Msiri alijinyakulia tuzo kadhaa katika tasnia ya uigizaji moja ikiwemo ya Sanaa Awards aliyotuzwa mwaka wa 2018.

 Mashabiki kwenye mitandao ya kijamii wametuma rambi rambi zao kwa familia, jamaa na marafiki.



By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post