Na Mwandishi wetu
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)Mkoa wa Morogoro, Dorothy Mwamsiku amempongeza Rais wa Tanzania ambaye pia Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa,Samia Suluhu Hassan kwa kukikubeba Chama chao kuwalea na kuwapa heshima katika kila nyanja ndani na nje ya nchi.
Pia amezitaka kata 14 za Manispaa ya Marogoro kuhakikisha zinaweka mipango ya uwanzishwaji wa miradi ndani ya kata na kuhakikisha wanajenga majengo ya Kupendeza ya Ofisi zao za Chama kwani ndio nembo ya Chama chao.
Amezungumza hayo wakati wa kuanza ziara yake ya kutembelea majimbo mbalimbali katika mkoa huo kwa lengo la kushukuru kuchaguliwa kwake kuwa Mwenyekiti wa Mkoa huo,Mwamsiku ambapo kutokana na kuongozwa na Rais mwanamke,ni vema wanawake wasijute kuzaliwa wanawake kwani wanaona kazi zilizofanywa na mwanamke kiongozi huyo ni jambo la kujivunia.
Amesema kwa sasa wanawake wanaweza,kwani yeye ni Mwenyekiti wa Kwanza kuongoza Chama hicho ndani ya Chama cha CCM ndani ya mkoa huo,hivyo ni wakati sahihi wa wanawake kujivunia.
" Chama chetu mkoa wa Morogoro kinampongeza kwa dhati Rais Samia kuchaguliwa kwake kwa kishindo kwa asilimia 100 kuwa Mwenyekiti wa Chama Taifa,hivyo tunahaidi kuendelea kumpa ushirikiano dhabiti kuhakikisha anaendelea kutuongoza vema,"amesema na kuongeza
"Pia nawapongeza wajumbe wa Halmshauri kuu ya Taifa wa Chama chetu katika kuchaguliwa kwao na kuongoza jahazi la wanaccm Taifa,"alisema Mwamsiku
Amesema Uongozi ni Utumishi alipoamua kwenda kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya uwenyekiti ndani ya Chama chao mkoa wa Morogoro aliamua kuwatumikia wanachama wa Chama hicho na wale ambao sio wanachama wa Chama hicho akiwa Mtumishi wao.
Mwamsiku amesema hana kisasi wala malipizi kwani uchaguzi umeisha sasa kazi inaendelea ya kujenga Chama hivyo amehaidi atawatendea haki watu wote kwa kufata kanuni,katiba na Muongozo wa Chama chao na kuhaidi kufanya kazi nao kwa ushirikiano.
"Nitafata katiba ya Chama katika kutetea maslahi ya Chama ndani ya Mkoa wa Morogoro, na katika utendaji kazi wangu sitamuonea mtu yeyote wala kukata jina lake katika uchaguzi wa ndani ya Chama.
"Na naagiza Kamati ya siasa ya Wilaya kama kuna mwanachama atafanya kinyume na Sheria na taratibu pizza Chama lkimshughulikie kwa kufata Sheria na taratibu za Chama zilizopo kwa kupata ushahidi,"amesema.
Amesisitiza kazi kubwa ya kiongozi ni kuwa na sikio sikivu hivyo watu waache makundi ndani ya mkoa wake kwani uchaguzi umekwisha sasa ni kazi ya kujenga Chama na Manispaa yao.
Aidha amesema hawawezi kuwa Chama kikubwa Duniani kama hakijakaa vizuri katika miundombinu yake ,ameagiza ifikapo Disemba mwaka huu Kata 14 kati ya kata 29 za manispaa ya Morogoro kuhakikisha zinakuwa na mipango ya kuweka miradi imara na kujenga Ofisi Nzuri za Chama .
"Sitaki kuona kata isiyona Ofisi ya CCM,nataka kata zote ziwe na Ofisi na miradi pia iwe imara,tuna kata 29 kati ya hizo kata 15 ndio zenye miradi mikubwa na Ofisi nzuri,nitapambana kwa nguvu zote kata zote ziwe na Ofisi za kupendeza kwani ndio nembo ya Chama,"amesema Mwamsiku.
By Mpekuzi
Post a Comment