Rais Dk.Mwinyi Akabidhiwa Ripoti Ya CAG Zanzibar |Shamteeblog.

 


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ameahidi kwamba hatua kali zitachukuliwa kwa wale wote waliohusika na kasoro zilitolewa katika ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ili kasoro hizo zisije kurudiwa tena.


Rais Dk. Mwinyi aliyasema hayo jana  mara baada ya kukabidhiwa Ripoti za Hesabu za Serikali kwa mwaka 2019 -2020, huko katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar, hafla ambayo imehudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.


Rais Dk. Mwinyi alisema kuwa fedha nyingi za Serikali zinapotea kwa kiasi kikubwa na iwapo hali hiyo itaendelea maendeleo hayatoweza kupatikana katika kuijenga nchi.


Alisema kuwa  lengo na madhumuni ya kupokea ripoti hiyo hadharani ni katika suala zima la kuhimiza uwajibikaji na utawala bora kwani ni lazima Serikali iwe wazi na kujulikana changamoto ndipo itakapowezekana kukabiliana na matatizo kama hayo.


Aliongeza kwamba katika Taasisi za ukusanyaji wa fedha bado kuna upotevu wa udhaifu wa mifumo na hata dhamira ovu ya watendaji katika ukusanyaji wa fedha za Serikali.


Rais Dk. Mwinyi alisisitiza kwamba mbali ya suala la ukusanyaji pia katika Taasisi hizo kunaonekana kwamba kuna udhaifu wa matumizi ambalo nalo limepelekea upotevu mkubwa wa fedha za Serikali ambapo hata kile kidogo kinachokusanywa hakitumiki vizuri.


Alisema kuwa hali hiyo ni vyema ikawafanya wote wakatafakari na kufanya  ama kuchukua hatua za msingi za kudhibiti hali hiyo.


Hivyo, Dk. Mwinyi alisema kuwa haiwezekani ionekane kumepokewa tu taarifa hiyo bali ni lazima hatua zinazohitajika zikachukuliwa hasa ikizingatiwa kwamba fedha hizo zinahitajika katika kuimarisha miradi ya maendeleo.




By Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post