Sasa ni rasmi pambano la ngumi kati ya mabondia wawili waingereza Anthony Joshua na Tyson Fury litafanyika Agosti 14 mwaka huu huko Saudia Arabia, kwenye uwanja maalumu utakao tengenezwa mahususi kwa pambano hilo, amethibitisha Promota Eddie Hearn.
Hearn ambaye ni promota wa AJ amethibitisha kuwa makaubaliano ya pambano hilo yamefikiwa, ingawa bdo upande wa bondia Tyson Fury haijathibitisha kufikia makubaliano ya kufayika kwa pambano hilo.
kuhusu uwanja utakao tumika kwa pambano hilo Hearn amesema; “Wanataka kujenga uwanja mpya. Wanataka kuunda kitu maalum sana mara ya mwisho waliunda uwanja wa pambano la Andy Ruiz Jr na AJ ndani ya wiki saba tu.
Wana nafasi ya kutumia viwanja vya ndani lakini wanataka kuunda kitu ambacho kitashtua ulimwengu, wanataka kujenga uwanja kwa ajiri ya pambano hili tu.”
Pambano hili linatajwa kuwa ni pambano kubwa katika historia ya mchezo wa masumbwi Uingereza, kutokana na uora wa mabondia waote ikiwemo kushikiria mikando yote ya uzani wa juu.
Anthony Joshua anashikilia mikanda minne ya uzito wa juu ambayo ni IBF, WBA , IBO na WBO na Tyson Fury anashikilia mkanda wa WBC.
Joshua ameshinda mapambano 24 kati ya mapambano 25 aliyocheza akiwa amepoteza pambano moja tu, wakati Tyson Fury hajawai kupoteza pambano hata moja kati ya mapambano 31 ameshidna 30 na pambano moja lilimalizika kwa sare.
from Author
Post a Comment