Mvutano baina ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Sipora Liana na Meya wake Songoro Mnyonge, umemalizika baada ya Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla kuingilia kati.
Liana na Mnyonge walitoleana maneno makali kwenye moja ya kikao cha Baraza la Madiwani kutokana na kuwepo kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za makusanyo mbalimbali.
Mapema leo Ijumaa, Makalla aliwaita kwenye kikao maalumu viongozi hao na kuzungumza kwa lengo la kumaliza mvutano huo, ambapo muafaka ulipatikana. Pia, aliwataka kwenda kufanya kazi ya kuwaletea maendeleo wananchi wa Kinondoni waliyotumwa.
Kwa upande wa Meya na Mkurugenzi wamemaliza tofauti zao na wamehaidi kufanya kazi kwa pamoja kwa maslahi mapana ya Wananchi.
By Mpekuzi
Post a Comment