SATF yawafunda walimu umuhimu wa kumlinda mtoto shuleni |Shamteeblog.

 Na Mwandishi wetu, Songea


TAASISI ya Social Action Trust Fund (SAFT) inayojihusisha kuwasaidia  watoto walio katika mazingira magumu  kupata elimu,huduma za  afya ya msingi kupitia Bima ya Afya ya jamii, imetoa mafunzo  ya kumlinda mtoto  kwa walimu sitini (60) wa shule za sekondari kutoka mikoa minne ya Lindi,Ruvuma,Mtwara na Njombe.

Meneja wa mradi wa SAFT  Bwana Nelson  Rutabanzibwa amesema kuwa, wameamua kuja na mpango wa  kutoa mafunzo kwa walimu ambao wao ndiyo walezi wa watoto hawa wawapo shuleni ili kuhakikisha  watoto wanapata haki zao za msingi.

Alisema, taasisi ya SAFT  iliyoanzishwa  kwa ushirikiano kati ya serikali ya Marekani  na serikali ya Tanzania mwaka 1998 hadi sasa  inafanya kazi kwenye mikoa 16 na Halmashauri  34 za Tnzania, lengo  ni  kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu,  kwa kuwawesha kupata elimu kuanzia ngazi ya elimu ya msingi, sekondari hadi vyuo ikiwemo vyuo vya ufundi, pia SATF inawawezesha watoto kupata huduma ya Afya ya msingi, ulinzi na haki za mtoto na kuziwezesha kiuchumi kaya masikini ziweze kuwapatia mahitaji muhimu watoto hawa.

Mafunzo hayo yaliyofanyika mjini Songea pia yalihusisha na taasisi mbalimbali kama vile LIWOPAC kutoka Lindi, FAWOPA kutoka Mtwara, JEUMA na SAFINA kutoka Njombe pamoja na GSM kutoka Ruvuma.

Akifungua mafunzo hayo Katibu Tawala wa mkoa wa Ruvuma  Steven Mashauri Ndaki, amelipongeza shirika la SATF kwa kuanzisha utaratibu huu wa kutoa elimu ya malezi na  vitendo vya ukatili dhidi ya watoto wadogo na kuwataka walimu waliobahatika kushiriki mafunzo hayo kwenda kuifanyia kazi elimu walioipata.

Baadhi ya walimu wameipongea  taasisi hiyo kwa kutoa elimu kwa walezi wa watoto hasa wawapo mashule kwani itawasaidia watoto walio kwenye mazingira magumu kupata haki za msingi.

Mwalimu Emmaculat Ngonyani mshiriki kutoka Wilaya ya Nyasa amesema kuwa, kupitia  mafunzo hayo amepata faida nyingi ikiwemo namna mtoto anavyopaswa kupewa mahitaji muhimu. Lakini pia kumsaidia kukabiliana na changamoto zinazotokana na rika barehe kama vile mimba za utotoni zinazopelekea watoto kuacha shule

“faida ambazo nimezipata kwenye mafunzo ya leo ni hasa kama ulinzi wa mtoto, kwa kuwa mtoto anahitaji ulinzi, kuheshimiwa, kupewa mahitaji muhimu, lakini pia  kutengenezewa mazingira yaliyo salama ili aweze kusoma na kuishi vizuri
 na faida nyingine ni matunda ya matokeo ya kile tunachoenda kukifanya huko mashuleni kwetu"alisema.

Mwalimu Yusuph Madande wa shule ya shule ya sekondari Lindi mkoa wa Lindi, amefurahishwa na mafunzo haya kwa kuwa yamempa somo yeye kama mwalimu na mzazi  jinsi ya kumsaidia mtoto hasa wa kike anapokuwa kwenye uhitaji  pindi wanapovunja ungo.

“ni taasisi chache sana zinatoa mafunzo kwa walimu wa kiume kuhusiana na mtoto wa kike ,hivyo kwa mafunzo haya tuliyoyapata tumejengewa uwezo wa kuwasaidia watoto wa kike hasa pale wanapofikia kwenye siku zao (hedhi), hasa kwa zile shule ambazo hazina walimu wa kike”

Kwa Upande wake Kaimu afisa elimu wa mkoa wa Ruvuma Mussa Mkoramigwe ameipongeza taasisi hii ya social Action trust fund (SATF) kwa kutoa elimu kwa walimu, namna ambavyo wanatakiwa kuwajibika kwa kuwalea wanafunzi  hasa juu ya matunzo ya mtoto na kudhibiti ukatili kwa watoto.

Walimu wa kutoka mikoa ya  Lindi, Njombe, Ruvuma pamoja na Mtwara katika halmashauri zinazotekeleza na mradi huu satf wamepata mafunzo ya namna ya kuwalea watoto ambao ni wanafunzi waliopo katika shule  za mikoa hiyo  minne ili kuwapa walimu elimu juu ya ukatili na mfunzo ya mtoto.

Amewakumbusha walimu  hao, kuhakikisha kila shule inakuwa na vilabu  ili kuwawezesha wanafunzi kushiriki katika masuala mbalimbali ikiwemo usafi na utunzaji wa mazingira  ili kuleta  mabadiliko makubwa  katika malezi y watoto wa kike na ushauri juu ya hedhi salama.

Meneja wa mradi wa SAFT  Bwana Nelson  Rutabanzibwa akitoa mafunzo kwa walimu 60 walioshiriki  mafunzo ya namna kuwalinda watoto yaliyoendeshwa na shirika hilo  Mjini Songea.


Meneja wa mradi wa SAFT  Bwana Nelson  Rutabanzibwa akitoa mafunzo kwa walimu 60 walioshiriki  mafunzo ya namna kuwalinda watoto yaliyoendeshwa na shirika hilo  Mjini Songea.



Mgeni rasmi Katibu Tawala wa mkoa wa Ruvuma  Steven Mashauri Ndaki,akiwa katika picha ya pamoja na walimu 60 walioshiriki mafunzo ya kumlinda mtoto yaliyotolewa na Shirika la SATF mjini Songea.



Meneja wa mradi wa SAFT  Bwana Nelson  Rutabanzibwa akitoa maelezo ya awali kuhusu mpango wa  kutoa mafunzo ya kuwalinda watoto kwa walimu  Mjini Songea. katikati ni Katibu Tawala wa mkoa wa Ruvuma  Steven Mashauri Ndaki, na kushoto ni Kaimu afisa elimu wa mkoa wa Ruvuma Mussa Mkoramigwe.


By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post