SERIKALI YAAHIDI KUFANYA KAZI KWA UKARIBU NA JUKWAA LA WAHARIRI NCHINI |Shamteeblog.

 



Mkutano mkuu wa sita na mkutano wa 10 tangu kuanzishwa kwa jukwa la wahariri. Umehudhuliwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa leo 20 Mei 2021 mjini Morogoro katika mkutano wa 6 wa jukwaa la Wahariri nchini kilichobeba kauli mbiu ya “Vyombo vya Habari kwa Maendeleo” Jukwaa la Wahariri linehudhuliwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa ambapo alikuwa Mwenyeji wake katika kikao hicho.

Mhe. Bashungwa amewahakikishia Jukwaa la habari kufanya nao kwazi kwa ukaribu kwa manufaa ya kujenga Taifa lenye mshikamano na umoja katika kuendeleza dira ya Maendeleo ya nchi.

“Serikali kupitia Wizara ninayoiongoza imeendelea kushirikiana vema na vyombo vya habari hapa nchini ili kuviwezesha vyombo hivyo pamoja na waandishi wa habari kutekeleza majukumu yao bila vikwazo huku wakizingatia Sheria, Kanuni, weledi na maadili ya uandishi wa habari.”

Waziri Innocent Bashungwa aliongeza kwa kusisitizia juu ya kuundwa kwa bodi ya ithibati ambayo itategemea kwa kuundwa kwa baraza huru la Habari Nchini.
“Kuundwa kwa Baraza hili kunategemea kuundwa kwa Bodi ya Ithibati kwa sababu wajumbe wa Baraza hili ni Waandishi wa Habari waliopewa Ithibati na Bodi ya Ithibati.”

“Wizara ishaanza mchakato kwa kuundwa kwa Bodi na ilishawasilisha mapendekezo ya majina ya wajumbe wa Bodi kwa ajili ya upekuzi.”


Nae Mgeni Rasmi Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka  wahariri wa vyombo vya habari  wahakikishe wanazingatia weledi na maadili katika uandishi wa habari  ili umma uweze kupata habari zenye ubora.

Amesema kuwa utendaji unaozingatia weledi ni chachu ya kuimarisha uhuru wa vyombo vya habari na wamiliki wake.

“kaulimbiu yenu ya Vyombo vya Habari na Maendeleo inahamasisha uandishi wa uwajibikaji. Vyombo vya habari vinapaswa kutambua katika kila habari vinayoiandika kuwa nyuma yake kuna masilahi ya taifa. Visipofanya hivyo, upotoshaji unaweza kuigawa nchi yetu, kuhatarisha amani na mshikamano wetu”.

Vile vile Waziri Mkuu ameviasa vyombo vyote vya  habari nchini kuhakikisha vinatanguliza Uzalendo, Utaifa na Maslai ya Nchi katika kufanya kazi “Mjenga Nchi ni Mwananchi. Hakuna mwingine zaidi yenu wa kulisemea Taifa letu”

Aidha Waziri Mkuu Kasim Majaliwa amesema kuwa Serikali haitamvumilia mtu yeyote atakayewakwaza mwandishi wa habari wakiwa katika utekelezaji wa majukumu yao.

Waziri Mkuu pia ameziagiza Wizara na Idara zote za Serikali ambazo hazijalipia matangazo zifanye hivyo mara moja ili kuviwezesha vyombo hivyo kujiendesha.

Waziri Mkuu ameiagiza Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, kukamilisha mchakato wa kuundwa kwa Bodi ya Ithibati ya Habari itakalofanya kazi ya kusimamia maadili ya taaluma ya uandishi wa habari ili kuwezesha uundwaji wa Baraza Huru la Habari.

Nae Kaimu Mwenyekiti wa jukwaa la wahariri Balile alianza kwa kutoa lisala akimshukuru waziri mkuu kwa kufungua mkutano mkuu wa wahariri wenye kauli mbiu “Vyombo vya Habari na Maendeleo” amao unalenga katika kuhabarisha umma juu ya kutangaza mipango na maendeleo ya kitaifa pamoja na Miradi ya serikali.

Tunaomba serikali kupitia wizara ya habari kutushirikisha kikamilifu katika mipango ya maendeleo nchini ili kuweza kuisemea Serikali vizuri na Pia wamemshukuru mheshimiwa waziri kwa kuonyesha hari ya kuzipitia tena sheria kandamizi za vyombo vya habari. Alikutana na wamiliki wa magazeti yaliyofungiwa kwa muda mrefu kutokana na agizo la Mhe. Samia Suluhu Hassan kuvifungulia vyombo vya habari Nchini.


By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post