SPIKA NDUGAI AWAAPISHA WABUNGE WAPYA WA MAJIMBO YA BUHIGWE, MUHAMBWE |Shamteeblog.

Charles James, Michuzi TV

SPIKA wa Bunge, Job Ndugai amewaapisha wabunge wawili wapya kutoka mkoani Kigoma ambao ni Dk Florence Samizi wa Jimbo la Muhambwe na Kavejuru Felix wa Jimbo la Buhigwe wote wanatokana na Chama Cha Mapinduzi CCM.

Wabunge hao wamechaguliwa kuwa wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi mdogo uliofanyika katika majimbo hayo Mei 16 mwaka huu.

Dk Florence Samizi wa Jimbo la Muhambwe amechaguliwa kufutia kifo cha aliyekua Mbunge wa Jimbo hilo, Mhandisi Atashasta Nditiye ambaye alifariki Dunia kwa ajali ya gari akiwa jijini Dodoma.

Kwa upande wake Mbunge wa Buhigwe, Kavejuru Felix amechaguliwa kuwa Mbunge kufuatia aliyekua Mbunge wa Jimbo hilo, Dk Philip Mpango kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
SPIKA wa Bunge, Job Ndugai akimuapisha Dk Florence Samizi wa Jimbo la Muhambwe
SPIKA wa Bunge, Job Ndugai akimuapisha Mbunge wa jimbo la Buhigwe, Kavejuru Felix





By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post