TMDA YATOA MAFUNZO KWA WATUMISHI WA AFYA |Shamteeblog.


Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Aziza Mumba akiwa katika picha ya pamoja na watoa huduma wa afya kutoka Halmashauri zote za Mkoa wa Dodoma Mara baada ya kumalizika kwa mafunzo yaliyotolewa na TMDA juu ya matumizi mabaya ya dawa na vifaa tiba.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Aziza Mumba akizungumza wakati wa kufungua mafunzo juu ya matumizi mabaya ya dawa na vifaa tiba. Mafunzo hayo yametolewa na TMDA kwa watoa huduma wa afya kutoka Halmashauri zote za Mkoa wa Dodoma.
Washiriki mbalimbali wa mafunzo juu ya matumizi mabaya ya dawa na vifaa tiba ambao ni watoa huduma wa afya kutoka Halmashauri za Mkoa wa Dodoma wakifuatilia mafunzo hayo.


Charles James, Michuzi TV

KATIKA kupunguza matumizi mabaya ya dawa na vifaa tiba, Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Nchini (TMDA)   imetoa mafunzo kwa watoa huduma wa afya kwa lengo la utoaji taarifa huku pia mamlaka hiyo ikikumbushwa kuendelea kutoa elimu kwa jamii juu ya matumizi mabaya ya dawa na vifaa hivo.

Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo jijini Dodoma, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Aziza Mumba ametoa wito kwa TMDA kuendelea kutoa elimu juu ya matumizi sahihi ya dawa na vifaa tiba kwa jamii.

Kaimu RAS, Mumba amesema lengo kubwa la kutoa mafunzo hayo ni kuhakikisha madhara makubwa juu ya athari ya dawa kwa watumiaji inapungua hivyo kutaka mafunzo hayo yawe ni endelevu zaidi.

Ametoa wito kwa mamlaka hiyo ya TMDA kuendelea kutoa elimu kwa wananchi na jamii kwa ujumla ili iweze kuelewa vifaa tiba na dawa wanazotumia mbali na matokeo chanya lakini zinaweza kuwa na matokeo hasi kwenye miili na afya zao.

" Niwapongeze TMDA kwa mafunzo haya na niwasihi taarifa ziwe zinaenda kwa haraka ili kudhibiti matumizi ya dawa ambazo zina madhara kwa mwanadamu na suala hili ni pana sana hivyo elimu zaidi inahitajika," Amesema Mumba.

Mafunzo hayo yamelenga kutoa elimu kwa watumishi wa sekta ya afya kutoka katika Halmashauri za Mkoa wa Dodoma ili kuwakumbusha msingi Mkubwa wa utoaji wa taarifa ambazo zinasaidia maisha ya binadamu.

" Niwaisihi kutumia taaluma zetu kuwalinda wananchi wetu, ninaamini mafunzo haya yatakua msaada mkubwa siyo kwenu pekee bali na kwa wananchi wetu katika Halmashauri tunazotoka," Amesema Mumba.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa TMDA Kanda ya Kati, Sonia Henry amesema mafunzo hayo yanahusisha watumishi takribani 30 kutoka Halmashauri zote za Dodoma huku akiwasihi watumishi hao kutumia mafunzo hayo katika kuisaidia pia jamii.



By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post