Watu wapatao 20 wamekufa na wengine watano hawajulikani waliko baada ya hali mbaya ya hewa kuwaathiri wanariadha waliokuwa wakishiriki mbio za kilomita 100 milimani nchini China.
Maafisa wa serikali wamesema.Shirika la habari la serikali nchini humo (Xinua) limesema mvua ya mawe iliyoandamana na theluji na upepo mkali iliwanyeshea wanariadha wakishiriki mbio hizo katika msitu karibu na mji wa Baiyan, kaskazini magharibi mwa mkoa wa Gansu.
Shirika la Xinua limesema waokoaji 700 wametumwa kuwatafuta wanariadha ambao hawajulikani waliko.
Wanariadha waliathiriwa kufuatia kushuka ghafla kwa viwango vya joto kutokana na hali hiyo ya hewa iliyobadilika.
Wanariadha wengine 151 wamethibitishwa kuwa salama na wengine watano wanaendelea kutibiwa hospitalini.Tukio hilo lilitokea jana mchana.
from Author
Post a Comment