WAZIRI LUKUVI AIKABIDHI KOM GROUP OF COMPANIES LTD NYARAKA UMILIKI ENEO LA KIWANDA CHA KUCHAKATA NYAMA ZA KUKU |Shamteeblog.
Kampuni ya KOM Group Of Companies Limited ya Mjini Kahama mkoani Shinyanga leo Jumatatu Mei 10,2021 imekabidhiwa nyaraka za kumiliki eneo la heka 100 kwa ajili ya uwekezaji wa Kiwanda cha kuchakata nyama za kuku na chakula cha mifugo katika eneo la Kibaha vijijini mkoani Pwani. Kushoto ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akikabidhi nyaraka hizo leo jijini Dodoma kwa Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya KOM Group Of Companies Limited Shija Felician (kulia).
Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya KOM Group Of Companies Limited Shija Felician (kulia) akionesha nyaraka za kumiliki eneo la heka 100 kwa ajili ya uwekezaji wa Kiwanda cha kuchakata nyama za kuku na chakula cha mifugo katika eneo la Kibaha vijijini mkoani Pwani. Kushoto ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi
By Mpekuzi
Post a Comment