WAZIRI MKUU MAJALIWA AAHIDI SERIKALI KUENDELEA KUWEKA SERA NZURI ZINAZOTOA FURSA KWA VYUO VYA UFUNDI NA SEKTA BINAFSI |Shamteeblog.


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof Joyce Ndalichako, manaibu mawaziri na watendaji wa NACTE baada ya kufungua maonesho ya pili ya elimu ya ufundi yanayofanyika jijini Dodoma.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa maonesho ya pili ya elimu na ufundi yanayofanyika jijini Dodoma leo.
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof Joyce Ndalichako akizungumza wakati wa ufunguzi wa maonesho ya wiki moja ya elimu ya ufundi yanayofanyika jijini Dodoma.
Wananchi na wanafunzi mbalimbali jijini Dodoma ambao wamejitokeza kwenye ufunguzi wa maonesho ya wiki moja ya elimu ya ufundi ambayo yamefunguliwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipatiwa maelezo katika banda la Chuo Cha Usafirishaji NIT wakati alipofika kuzindua maonesho ya wiki moja ya elimu na ufundi jijini Dodoma.


Charles James, Michuzi TV

SERIKALI imesema itaendelea kuweka sera nzuri zinazotoa fursa kwa Vyuo vya Ufundi na sekta binafsi ili kuhakikisha mafanikio yanapatikana.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati akifungua maonesho ya pili ya elimu ya ufundi yaliyoandaliwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) ambayo yamefanyika jijini Dodoma.

Waziri Mkuu Majaliwa ameitaka Wizara ya Elimu Sayasi na Teknolojia kuimarisha ushirikiano kati ya sekta binafsi ili kukuza ujuzi huo wa mafunzo na ufundi.

Amezihakikishia sekta binafsi ushirikiano huku akiwasisitiza kufika serikalini pindi wanapokutana na changamoto zozote waweze kupatiwa msaada wa kukabiliana na changamoto hizo kwani wote wanajenga nyumba.

Ametoa wito pia kwa wadau wote wa elimu na mafunzo ya ufundi kuungana na kushikamana na kuzungumza lugha moja kwa kuhakikisha mwelekeo huo unaeleweka kwa watanzania.

Waziri Mkuu Majaliwa ameongeza kuwa Serikali imeendelea kuimarisha mazingira ya kuwekeza nchini katika sekta ya elimu na kwamba hadi kufikia mwaka huu wa 2021 idadi ya Vyuo vilivyosajiliwa na NACTE ni 430.

" Idadi ya wanafunzi waliojiunga na Vyuo hivyo pia imeongezeka kutoka 117,478 mwaka 2015 hadi 172, 312 kwa mwaka jana 2020, na wanafunzi hao ni wa ngazi ya Astashahada na Stashahada na ni ukweli kwamba ongezeko hilo limepanua wigo kwa wahitimu wa kidato cha nne kujiunga na masomo katika ngazi hizo.

Lakini pia ongezeko hilo limetoa nafasi kwa vijana waliomaliza Darasa la Saba kujiunga na Vyuo vya Ufundi kama VETA na wale ambao hawajapata elimu kabisa kujiunga na taasisi ambazo zinatoa elimu ya ufundi na ujuzi ili waweze kushindana katika soko la ajira na wengine kujiajiri," Amesema Waziri Mkuu Majaliwa.

Kwa upande wake Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof Joyce Ndalichako amesema maonesho hayo yatakayodumu kwa wiki moja yatachochea ari ya pamoja baina yao kama Wizara na wadau wa sekta binafsi katika kubadilisha mawazo katika kuboresha utoaji wa elimu ya ufundi na teknolojia nchini.

Nae Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la NACTE, Prof John Kondoro amesema Baraza hilo litaendelea kusimamia utoaji wa mafunzo kwa ubora unaotakiwa ili kuweza kukidhi vigezo vinavyotakiwa katika soko la ajira za ushindani nchini.



By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post