CCM Yahimiza Watanzania Kulinda Amani Ya Nchi |Shamteeblog.


Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kinatambua na kuthamini mchango wa dini zote katika kuimarisha  na kuhuisha amani, umoja na mshikamano nchini.

Hivyo CCM  imewaomba watanzania kuendelea kuitunza, kuilinda na kuidumisha amani kwa vile maendeleo hayawezi kupatikana bila amani, mambo yote mazuri ili yafanyike ikiwemo ibada lazima amani iwepo kwanza hivyo  kila mmoja asikubali kwa namna yoyote kuona amani ya nchi  ikichezewa na kutoweka.

Akizungumza kwa Niaba ya Katibu Mkuu wa CCM, Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Ndugu Shaka Hamdu Shaka katika mkutano mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) mkoani hapa  amesema kazi ya kulinda na kuitunza amani ya nchi ni jukumu la kila raia mwema hivyo wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama kwa kuvipa taarifa juu ya uwepo wa mipango au viashiria vya kuhujumu amani au kutenda uhalifu ili hatua stahiki za kisheria zichukuliwe kwa wakati.

 "Mwenyezi Mungu katika Quran Suratul al Imran (103)  amesema  shikamaneni katika Kamba ya Mwenyezi Mungu,  wala msifarikiane kumbukueni neema ya allah iliyo juu yenu. katika Zaburi 133 (1) anasema tazama ilivyo vema na kupendeza,  ndugu wakae pamoja, kwa umoja. CCM inaipongeza  Serikali inayongozwa na Rais Samia kwa namna inavyoendelea kuwaunganisha watanzania bila kujali itikadi za kisiasa, kiimani na kikabila" Alisema Shaka

Shaka amefahamisha kuwa CCM kupitia ilani ya uchaguzi  ya mwaka 2020-2025  itaendeleza amani, umoja, usalama,  utawala wa sheria na utulivu wa kisiasa jambo ambalo litawezesha shuhuli zote za  kiimani  na kimaendeleo kufanyika nchini.

"Niwaombe watanzania wote tuendelee kumuombea  Rais wetu Mhe. Samia Suluhu Hassan na serikali anayoiongoza kuendelea kutuongoza kwa kuheshimu utawala wa sheria, haki na usawa ili amani yetu iendelee kudumu na nchi yetu ipige hatua zaidi kimaendeleo." Alifahamisha Shaka.

Mkutano huo umefunguliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango


By Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post