Fahamu Utajiri wa Kutupwa wa Marehemu T.B Joshua |Shamteeblog.

 


ULIMWENGU wa kiroho umegubikwa na simanzi kufuatia kifo cha aliyekuwa mhubiri wa kimataifa, T. B Joshua, kubwa zaidi linalozungumzwa ni juu ya utajiri wa kutisha aliouacha.

Kwa mujibu wa moja ya ripoti za Shirika la Habari la Uingereza BBC –Idhaa ya Kingereza, T. B Joshua anatajwa kumiliki kiasi cha Dola za Kimarekani kati ya milioni 10 hadi 15.

Ripoti kama hiyo pia ilitolewa na Jarida la Forbes –Africa walipokuwa wakikusanya orodha ya wachungaji matajiri zaidi barani Afrika mwaka 2011.

Utajiri huo unatokana na bidhaa zinazouzwa kupitia huduma zinazotolewa na kanisa lake la SCOAN zikiwemo maombezi, maji na mafuta ya upako ambavyo vinaaminika kutenda miujiza kwa kuponya watu na kuwaondolea shida mbalimbali.

Kwa utajiri huo,T B Joshua anamiliki kituo cha Televisheni cha Emmanuel TV, Pia anamiliki ndege binafsi (private jet) na magari ya kifahari kama Range Rover, Mercedes Benz, Toyota Land Cruiser V8 na mengine.

Mtumishi huyo wa Mungu ameacha mke, Evelyn Joshua na watoto watatu.

Stori  na Sifael Paul



from Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post