Katiba Mpya, Mikutano ya Kisiasa Nipeni MUDA Nijenge Uchumi |Shamteeblog.

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewasihi Watanzania kumpa muda wa kushughulikia masuala ya uchumi kabla ya kutazama masuala mengine ya katiba na mikutano ya kisiasa.

Rais Samia ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari nchini Tanzania ambao amekutana nao Ikulu ya Dar es Salaam.

Amewaomba Watanzania apewe muda kwanza ili kuisimamisha nchi kiuchumi kisha atashughulikia masuala mengine.

”Naomba nipeni muda kwanza nisimamishe nchi kiuchumi, tuite wawekezaji wawekeze, ajira zipatikane, halafu tutashughulikia masuala mengine.”

”Tutashughulikia katiba, tutashughulikia mikutano ya hadhara, wakati ukifika.” Alisema Rais Samia.

Hata hivyo amesema sasa wanaruhusu vyama vya Siasa kufanya mikutano na watu wao, mikutano ya ndani, kamati kuu zinakaa, Halmashauri kuu za vyama vya siasa vinakutana.

Sambamba na hilo wameruhusu pia wabunge kwenye maeneo yao kufanya mikutano ya hadhara.

”Uchumi wetu ni suala la maana zaidi kuliko mengine, sisemi kwamba katiba si ya maana, lakini ninaomba nipeni muda, niisimamishe Tanzania kiuchumi kwanza halafu tutatazama na mengine. Alifafanua Rais Samia.



from Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post