Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mataka (kushoto) na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde wakionja chai yenye mchanganyiko maalumu katika banda la wajasiriamali katika maonesho hayo.
RC Mtaka akipat maelezo kuhusu mashine ya kujaza juisi kwenye glasi kutokana na kiwango cha fedha ulizolipia ambayo imeundwa na Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT). Kushoto ni Mbunge wa Dodoma Mjini, Anthony Mavunde,
RC Mtaka akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa Barza la Nacte, pamoja na Mkurugenzi wa Uthibiti, Ufutliaji na Tathmini wa Nacte, Dkt.Jofrey Oneke.
Wananchi wakipata maelezo katika Banda la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) wa maonesho hayo.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mtaka akiulia jambo alipotembelea banda la Chuo cha Taifa cha Utalii.
RC Mtaka akitia saini kwenye kitabu katika banda la Nacte ambao washirikiana na TPSF kuandaa maonesho hayo.
Mtaka akizungumza na maofisa wa Nacte alipotembelea banda hilo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Jiji la Dodoma, Joseph Mafuru akiahidi kuwaalika wajasiriamali washiriki katika maonesho hayo ya ubunifu.
RC Mtaka akizungumza na vyombo vya habari baada ya kutembelea Maonesho hayo.
Katibu Mtendaji wa NACTE, Dkt, Adolph Rutayuga akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu maonesho hayo ambapo aliahidi maonesho ya mwakani kuyaboresha zaidi.RC
RC Mtaka akiangalia magazeti ya zamani yanayohifadhiwa na Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania.
RC Mtaka akitoa ushauri kwa maofisa wa Benki ya CRDB, kwamba kila mwaka Taasisi za fedha ziwe zinatenga bajeti ya fedha za kusaidia kuwadhamini wabunifu ili kuendeleza vipaji vyao.
RC Mtaka akiishauriTanesco kuja na mkakati wa kuboresha huduma ambapo mteja akinunua umeme uwe unawaka bila mteja kumlazimu kwenda kwenye mita kujaza tokeni.
Mtaka akiwa na Mbunge wa Dodoma Mjini, Anthoni Mavunde alipokuwa akikagua mabanda ya taasisi mbalimbali.
RC Mtaka akioneshwa mtungi wa gesi inayotumiwa mbadala ya mafuta.
Akiangalia mipira iliyotengezwa na kampuni ya hapa nchini.
Akiwa katika banda la Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
RC Mtaka akiangalia baiskeli a kubebea wagonjwa inayotumia umeme wa jua. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mbarali.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka amezishauri Benki na Taasisi za fedha kutenga fedha kwa ajili ya kuwadhamini wabunifu nchini ili kuendeleza vipaji vyao.
Ameyasema hayo alipotembelea Maonesho ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi yaliyoandaliwa kwa ushirikiano na Baraza la Tgaifa la Elimu na Mafunzo ya Ufundi (NACTE) Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), kwenye Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
Maonesho hayo yameshirikisha vyuo mbalimbali vya ufundi,benki na taassi za fedha, wajasiriamali na wabunifu wa aina mbalimbali. Mdau nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, RC Mtaka akitoa ushauri huo....
Imeandaliwa na Richard Mwaikenda
Mhariri Blog ya Taifa ya CCM
0754264203
By Mpekuzi
Post a Comment