TAASISI ZILIZOPEWA MAJUKUMU YA KUCHANGIA FCC, ZICHANGIE KWA WAKATI ILI SHUGHULI ZA FCC ZISIKWAME |Shamteeblog.

 



Waziri wa viwanda na biashara, Profesa Kitila Mkungo akiongea kwenye ufunguzi wa mktano wa tano wa Tume ya Ushindani Tanzania (FCC) uliofanyika Dar es Salaam. 28/06/202

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani Tanzania (FCC) , William Erio akielezea kilichomo katika rasimu ya mpango mkakati wa tano wa Tume ya Ushindani Tanznia (FCC). Dar es Salaam, 28/06/2020


*************************

Na John Marwa 

Wito umetolewa kwa taasisi zote zenye jukumu la kuichangia Tume ya Ushindani Tanzania (FCC) kufanya hivyo kwa wakati lengo likiwa ni kuiwezesha taasisi hiyo kutekeleza majukumu yake ya kimsingi bila kukwama.


Katika wakati huu sasa ambao uchumi unaendeshwa na soko huria, FCC imekuwa ni kiungo muhimu kati mlaji na wafanyabiashara, kwa kuhakikisha kunakuwa na ushindani katika kufanya biashara huku ikimlinda mlaji kwa kuhakikisha anapata bidhaa bora.


Hayo yameelezwa leo Juni 28, 2021 na Waziri wa Viwanda na Biashara, Profesa Kitila Mkumbo wakati akifungua kikao cha kupitia mpango mkakati wa tano wa Taasisi hiyo kilichofanyika jijini Dar es Salaam.


Profesa Mkumbo amesifu mpango mkakati wa FCC kwa namna ulivyoandaliwa huku ukiakisi dira ya maendeleo ya Taifa na Mpango wa tatu Maendeleo ya Taifa sanjari na kuakisi maono pamoja na maelekezo ya mkuu wa nchi ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa wakati huo.


"Mpango mkakati wa FCC ni mzuri, kwanza umeakisiwa ndani ya dira yetu ya maendeleo ya Taifa na Mpango wa Tatu Maendeleo ya Taifa. Pia umeakisi maono na maelekezo ya mkuu wa nchi" alisema Profesa Mkumbo 


Kando na hilo, Waziri Profesa Mkumbo ametumia fursa hiyo kuwatoa hofu wafanyabiashara wote kwa kusema kuwa, hivi sasa si kipindi tena cha uhodhi wa dola katika kuendesha shughuli za biashara, bali ni kipindi cha uhodhi wa sekta binafsi katika shughuli hizo. 


Akizungumzia changamoto zinazoikumba FCC, Waziri huyo amebainisha kuwa, wachangiaji ambao wameainishwa kisheria kuichangia taasisi hiyo wamekuwa hawafanyi hivyo kwa wakati pamoja na ucheleweshwaji wa huduma kwa mtazamo wa wananchi jambo ambalo kwa upande mwingine amesema ni la utaratibu. 


Vilevile Profesa Mkumbo ameitaka FCC kuwahimiza wafanyabiashara na wamiliki wa viwanda katika suala la kushindana kijumuia, kikanda na kimataifa kuliko kutazama pekee soko la ndani.


Awali akiongea Mkurugenzi Mkuu wa TFF, William Erio amesema, mpango mkakati huo ni wa tano tangu kuanzishwa kwa FCC huku ukirejea dira ya taifa huku ukiwa na malengo sita. 


"Mpango mkakati huu umepambanua masuala ya kumlinda mtumiaji na kudhibiti bidhaa bandia  kwa kufanya hivyo italeta ufanisi zaidi katika utendaji na kutuwezesha kukidhi matarajio ya serikali na wananchi kwa ujumla" 


Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa katika kikao hicho wameshirikisha wadau mbalimbali ikiwemo taasisi za Serikali, jumuiya ya wafanyabiashara lengo likiwa ni kupata mawazo yao na kuhakikisha kwamba mpango huo unakuwa ni shirikishi na unaotekelezeka ili  kuhakikisha nchi yetu inakuwa na ufanisi katika shughuli za biashara na uwekezaji. 


Tume ya Ushindani (FCC) ni chombo cha serikali cha kusimamia uchumi wa soko, ambapo usimamizi huo unazingatia misingi ya ushindani, kumlinda maji na udhibiti wa bidhaa bandia. Tume hii imeanzishwa chini ya kifungu namba 62 cha sheria ya ushindani namna nane ya mwaka 2003.





By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post