TGNP YAPONGEZA KASI YA RAIS SAMIA SIKU 100 |Shamteeblog.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Lilian Liundi 

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
 
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Lilian Liundi amepongeza mwelekeo wa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan akisema inazingatia masuala ya usawa wa kijinsia hali itakayosababisha maendeleo yaende kwa haraka.

Liundi ameyasema hayo leo Jumatatu Juni 28,2021 akizungumzia Siku 100 za uongozi wa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan wakati akifungua mafunzo ya Bajeti yenye mrengo wa kijinsia kwa waandishi wa habari na viongozi wa vituo vya taarifa na maarifa kutoka mikoa ya Shinyanga (Kiloleli – Kishapu) na Dar es salaam (Mabwepande, Saranga, Kivule na Majohe) yanayofanyika katika ukumbi wa TGNP Mabibo jijini Dar es salaam.

Mkurugenzi huyo wa TGNP amesema katika siku 100, serikali ya awamu ya sita imeonesha mwelekeo mzuri katika kuzingatia masuala ya usawa wa kijinsia.

“Suala la jinsia ni suala la maendeleo,ni suala la uchumi, ni suala la kila kitu, hivyo ni lazima tutoe kipaumbele. Uchumi umekuwa ukiyumba kutokana na masuala ya kijinsia kutopewa uzito. Tunatarajia kwa mwelekeo huu tunaokwenda nao katika awamu ya sita pia hata maendeleo yatakwenda kwa haraka”,amesema Liundi.

“Tumeona masuala ya usawa wa kijinsia kwenye uongozi ,ni kitu ambacho tumekizungumza kwa muda mrefu tangu mkutano wa Beijing na utekelezaji wa azimio la Beijing, awamu zilizopita zilifanya juhudi zake lakini awamu hii ya sita imekuja na juhudi ambazo ni tofauti, ambazo zinatusogeza mbele zaidi.

Kwa hiyo tukiona Kiongozi wa nchi anazungumza wazi wazi kwamba kwenye masuala ya uongozi atatoa kipaumbele pia kwa wanawake wenye uwezo. Na tumeona anachofanya, kwa upande wa Makatibu Tawala ameteua wanawake asilimia 48, hii inakuwa ni kwa mara ya kwanza. Hiki ni kitu cha kujivunia”,ameeleza Liundi.

“Hizi siku 100 ni za kusherehekea mafanikio ya serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wetu Mpendwa Mhe. Samia Suluhu Hassan amelipa kipaumbele suala la usawa wa kijinsia. Tumeona pia majaji ameteua wanawake asilimia 42.8, mabalozi asilimia 33.3 lakini pia wakuu wa wilaya asilimia 31”,amesema Liundi.

Amesema kutokana na hali hiyo hivi sasa kwamba mwendo uliopo ni wa tofauti, mambo yanaenda vizuri kinachotakiwa ni kutoa ushirikiano, wale waliochaguliwa na kuteuliwa waendelee kujitoa, wafanye kazi vizuri, kwa uaminifu, uadilifu ili kuonesha kwa vitendo kuwa wanawake wana uwezo wa ziada.

Aidha amefafanua kuwa serikali ya awamu ya sita imeanza kuonesha mabadiliko kwa kuangalia tunu za kuongoza taifa mfano masuala ya haki, kilimo chenye tija, demokrasia, usawa na uhuru wa vyombo vya habari, kuondoa umaskini na rushwa ikiwemo ubadhirifu wa mali za umma na ukusanyaji kodi usio na bughudha.

Kuhusu mageuzi ya kilimo ambapo mkulima mdogo, mwanamke ndiyo amebeba taifa katika uhakika wa chakula , Liundi ameshauri mwanamke asije akatupwa pembeni, kuwe na mikakati mahsusi ili kuhakikisha kuna ushiriki wa wakulima wadogo wadogo hususani wanawake waliopo kwenye maeneo ya pembezoni ambao wamekuwa wakiteseka kila siku huku akishauri wanawake wapewe kipaumbele zaidi kwenye elimu ya ujuzi kwenye vyuo vya ufundi.

“Lakini pia tumeona katika masuala ya madini,maji, elimu,afya uchumi, utalii, viwanda, teknolojia ya habari na mawasiliano vinatiliwa uzito wa kipekee kama vipaumbele vya maendeleo ya taifa, tunachotaka mwanamke asiachwe nyuma na serikali imeshaonesha nia watu wote watanufaika”,amesema Liundi.

Amesema madhumuni ya mafunzo hayo kwa waandishi wa habari na viongozi wa vituo vya taarifa na maarifa ni kuongeza na kuimarisha uelewa wa washiriki juu ya bajeti yenye mrengo wa kijinsia kwa sababu suala la kijinsia ni suala la maendeleo.

"Kwa hiyo tunapokuwa na utengwaji wa rasilimali ambazo zinaangalia mtazamo wa jinsia, makundi yote katika jamii yatafaidika na rasilimali za taifa na ndiyo maana tunatia msisitizo”,amesema Liundi.

“Tunajua kuwa Bajeti yetu ya taifa imepitishwa na Bajeti ikipitishwa tujue kuwa mwaka mzima tutatembea katika huo mgawanyo wa bajeti. Hivyo kama wananchi ni vizuri kufahamu ni kitu gani kimepita, vipaumbele gani vimepitishwa hali itakayosaidia kufuatilia hizo rasilimali zinatumikaje kwa kuzingatia makundi yote katika jamii”,ameeleza.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Lilian Liundi akizungumza  wakati akifungua mafunzo ya Bajeti yenye mrengo wa kijinsia kwa waandishi wa habari na viongozi wa vituo vya taarifa na maarifa kutoka mikoa ya Shinyanga (Kiloleli – Kishapu) na Dar es salaam (Mabwepande, Saranga, Kivule na Majohe) leo Jumatatu Juni 28,2021 katika ukumbi wa TGNP Mabibo jijini Dar es salaam. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Lilian Liundi akizungumza  wakati akifungua mafunzo ya Bajeti yenye mrengo wa kijinsia kwa waandishi wa habari na viongozi wa vituo vya taarifa na maarifa kutoka mikoa ya Shinyanga  na Dar es salaam 

Mwezeshaji katika mafunzo ya Bajeti yenye mrengo wa kijinsia kwa waandishi wa habari na viongozi wa vituo vya taarifa na maarifa kutoka mikoa ya Shinyanga  na Dar es salaam, Deogratius Temba akitoa mada kuhusu Bajeti ya Mrengo wa Kijinsia.
Afisa Habari wa TGNP, Monica John akizungumza wakati mafunzo ya Bajeti yenye mrengo wa kijinsia kwa waandishi wa habari na viongozi wa vituo vya taarifa na maarifa kutoka mikoa ya Shinyanga  na Dar es salaam 
Washiriki wa mafunzo ya Bajeti yenye mrengo wa kijinsia ambao ni waandishi wa habari na viongozi wa vituo vya taarifa na maarifa kutoka mikoa ya Shinyanga  na Dar es salaam wakiwa ukumbini.

Washiriki wa mafunzo ya Bajeti yenye mrengo wa kijinsia ambao ni waandishi wa habari na viongozi wa vituo vya taarifa na maarifa kutoka mikoa ya Shinyanga  na Dar es salaam wakipiga picha ya kumbukumbu.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post