Wabunge Wataka Luku za Maji (Mita za Malipo ya Kabla) Ziharakishwe |Shamteeblog.



*Waipongeza Wizara ya Maji kwa kuliwekea mkazo suala hilo

*Wasema ndiyo mwarobaini wa kumaliza malalamiko ya bili za maji

*Majaribio kuanza nyumba za wabunge kati ya Julai hadi Septemba  mwaka huu

Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji wameipongeza Wizara ya Maji kwa kulipa msukomo suala la mita za malipo ya kabla (Prepaid Meters) na kuitaka kuharakisha suala hilo ili kuondoa malalamiko ya wananchi kuhusu bili kubwa za maji na bili bambikizi.

Wajumbe hao wamesema hayo wakati wakichangia katika kikao cha Kamati hiyo na Watendaji wa Wizara akiwemo Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, Naibu Waziri wa Maji, Maryprisca Mahundi, Katibu Mkuu wa Maji, Mhandisi Antony Sanga, na Naibu Katibu Mkuu, Mhandisi Nadhifa Kemikimba, kuhusu masula ya Ankara za maji.

Akichangia mjadala huo Mbunge wa Arusha Mjini, Mrisho Gambo, alisema anaipongeza Wizara kwa hatua hiyo na kusema kuwa maamuzi hayo yamechelewa sana.

Kwa Upande wake naibu Waziri wa maji Mhandisi Maryprisca Mahundi ameeleza kuwa wananchi watakaokuwa wanatumia huduma hiyo ni wale wale wa maisha ya kawaida na wa chini kama ilivyo kwa luku za umeme.

Akizungumza mara baada ya kusikiliza maoni ya Wabunge,Waziri wa Maji, Jumaa Aweso aliwatoa hofu wabunge kuhusu utekelezaji wa suala hilo na kusema pamoja na kwamba mwanzo huwa unatia hofu lakini hawana sababu ya kuogopa.

Aidha Waziri Awesso amependekeza  utaratibu wa mita hizi kuanza na viongozi wa Serikali na Wabunge ili iwasaidie kujifunza namna ya kwenda kuutekeleza kwa wananchi.



By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post