Balozi Sokoine: Wafanyabiashara Tumieni Balozi Za Tanzania |Shamteeblog.


Na Mwandishi wetu, Dar
Wafanyabiashara nchini wanaofanya biashara nje ya nchi wameshauriwa kuwasiliana na balozi za Tanzania ili kupata taarifa sahihi kuhusu fursa za biashara na uwekezaji katika nchi wanazopenda kufanya nazo biashara.

Wito huo umetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine wakati alipotembelea Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.

Balozi Sokoine amesema kuwa endapo wafanyabiashara watatumia Balozi za Tanzania Nje ya Nchi itakuwa rahisi kwao kuwapatia taarifa sahihi zaidi kuliko kutumia vyanzo vingine.

“Endapo wafanyabiashara wetu wanaofanya biashara nje watatumia fursa ya kuwasiliana na Wizara ya Mambo ya Nje kupitia Balozi zake Nje ya Nchi watapatiwa taarifa sahihi ambazo zitawasaidia kuokoa muda na kupata bidhaa kwa wakati,” Amesema Balozi Sokoine.

Pamoja na mambo mengine, Balozi Sokoine amewasihi watanzana kwa ujumla kupita katika banda la Wizara ya Mambo ya Nje ili kuweza kupata uelewa wa taarifa/ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya kidiplomasia.




By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post