DKT. SENGATI ATOA SIKU TATU UCHUNGUZI VYUMBA VYA MADARASA KISHAPU |Shamteeblog.
Na Anthony- Ishengoma.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati ametoa siku tatu kwa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Bw. Joseph Mkude kuhakikisha anafanya uchunguzi kuhusu kuchelewa kwa kuanza mradi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa katika Shule ya Sekondari Kishapu wenye thamani ya Sh. Milioni 40.
Dkt. Philemon Sengati alitoa agizo hilo wakati wa ziara yake inayoendelea Mkoani Shinyanga kwa lengo la kujionea miradi ya ujenzi inayotekelezwa kwa fedha za mradi wa EP4R nakubaini kuwa tofauti na maeneo mengine ujenzi wa vyumba hivyo vya madarasa katika shule hiyo bado unasuasua.
Kufuatia hali hiyo Dkt. Sengati akatoa agizo hilo kwa Mkuu wa Wilaya hiyo hili kubaini wale wote waliosababisha kusuasua kwa ujenzi huo hili hatua ziweze kuchukuliwa lakini pia kubaini kama fedha hizo bado zipo ili kukamilisha ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa kama ilivyo kwa shule nyingine zinazotekeleza mradi huo na ziko katika hatua nzuri za ujenzi.
Aidha pamoja na agizo hilo kwa Wilaya Kishapu Dkt. Sengati pia ametoa rai yake kwa wanafunzi wa shule mbalimbali katika maeneo aliyotembelea kuhakikisha wanajipanga kukabiliana na majanga ya moto kwa kutoa taarifa kama wanafununu yoyote ya mtu katika jamii anayepanga kufanya njama hiyo ili uwekwe utaratibu wa kukabiliana naye kabla hajatekeleza mpanga huo mbaya.
Dkt. Sengati amewataka wanafunzi hao kuchunguzana na kubaini kama kuna mwanafunzi mwenye hisia za kigaidi ili watoe taarifa kwa viongozi wa shule na kuwataka baadhi yao kubaki katika mabweni wakati wa maandalizi ya masomo ya jioni na anatoa tahadhari hiyo kufuatia baadhi ya shule mbalimbali kupata majanga ya moto hapa nchini.
Aidha kiongozi huyo wa Mkoa anatoa tahadhari hiyo kuwakumbusha wananchi na wanafunzi wa Mkoani Shinyanga kuwa tayari Mikoa ya Kilimajaro, Pwani na Morogoro zimapata majanga ya moto hivyo ni vyema mkoa wake ukachukua tahadhari mapema ili husije ukaingia katika majanga kama hayo.
Naye Mkuu wa Shule ya Msingi Old Shinyanga Mwalimu Joyce Julius katika taarifa yake kwa Mkuu wa Mkoa alisema shule yake tayari imeisha pokea milioni 40 za EP4R na tayari vyumba vya madarasa hayo viko katika hutua za Mwisho kukamilika na kuongeza kuwa kiasi cha fedha kilichobaki kinatosha kukamilisha ujenzi kwa hatua zalizobakia kwa kipindi cha mwezi ujao kwa kutumia akaunti ya dharula.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Bw. Geofrey Mwangulumbi amemwambia Mkuu wa Mkoa kuwa katika baadhi ya miradi inayoendelea na ambayo tayari nguvu ya wananchi imetumika Manispaa yake itaendelea kujipanga kumalizia miradi hiyo kutokana na mapato yake ya ndani na tayari wamejipanga kuongeza ufaulu ili Shinyanga iwe katika mikoa bora inayofanya vizuri kitaifa.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga anaendelea na ziara yake katika Wilaya za Mkoa wa Shinyanga na tayari amefanya ziara kama hiyo katika Wilaya ya Kishapu na ataendelea na ziara kama hiyo Wilayani kahama kukagua miradi ya maendeleo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ikiwemo miradi inayotekelezwa kwa fedha za miradi ya EP4R.
By Mpekuzi
Post a Comment