Baada ya kutangazwa kwa matokeo ya kidato cha 6 na Baraza la mitihani nchini Tanzani Shule za serikali zimeendelea kuongoza ukilinganisha
Lakini miamba ya matokeo mazuri ya mchepuo wa sayasi kwa upande wa shule binafi Feza na Canosa bado wameendelea kuonesha umwamba wao katika matokeo hayo.
Akizungumza na wandishi wa habari Mwalimu wa Taluma wa shule ya Feza Boys Richard Mahina alisema baada ya matokeo ya miaka miwili nyuma kuwa na ushindani mkubwa uongozi wa shule za Feza uliamua kukaa chini na wanafunzi na kukubaliana kuwa mwaka huu iwe isiwe lazima wairudishe FEZA kwenye njia nafasi zake
"Pia tulikubaliana kusoma kwa namna tatu 1 WAWAPO DARASANI ,WAKIWA NYUMBANI NA KWENYE MAGROUP MABLI MBLI ili kuweza kujijengea hali ya kujiamini kukabiliana na mitihani na matokeo yake ndio haya tumeingia top ten wanafunzi wawili na Shule imefanikiwa kushika nafasi ya sita kitaifa ni jambo la kujivunia'',alisema Mhina.
Kwa upande wa wanafunzi waliofanya vizuri katika Masomo ya sayansi, Harry Mshana na John Bugeraha walisema sababu kubwa iliyowafanya wafanye vizuri katika matokeo hayo ni U TATU MTAKATIFU yaani Waalimu ,Wazazi na Wanbafunzi
Kuna kipindi walimu walitutaka tuwepo shuleni hasa kipindi cha likizo na sikukuu lakini wazazi walikuwa wazito kuturuhusu baada ya majadiliano kwa pamja tulikubaliana Hakuna kulala hakuna kupumzika mpaka kieleweke na leo ndo faida ya kupambana darasani umeiona.
Wanafunzi wa shule ya Feza Boys wakishangilia kwa kuwabeba wanafunzi wenzao waliofanya vizuri matokeo ya kidato cha sita na kuingia kumi bora , Harry Mshana na John Bugeraha na kusababisha shule yao kushika nafasi ya sita (6) kitaifa mara baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo.Na mpiga picha wetu
Viongozi na waalimu wa shule ya Feza Boys wakiwapongeza wanafunzi waliofanya vizuri matokeo ya kidato cha sita kwa kuingia katika kumi bora , Harry Mshana(kulia) na John Bugeraha na kusababisha shule yao kushika nafasi ya sita (6) kitaifa mara baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo.Na mpiga picha wetu
By Mpekuzi
Post a Comment