Kwa takribani robo karne sasa bado dunia imeshindwa kubaini wauaji wa wakongwe wa Hip Hop duniani Tupac na Notorious B.I.G licha ya kuwepo kwa nadharia mbali mbali. Marehemu Notorious B.I.G maarufu Biggie amekuwa akituhumiwa kuhusika na mauaji ya Tupac kwa kuajiri mtu ambaye alienda kumwagia risasi Tupac mwaka 1996.
Mwaka mmoja uliofuata Biggie naye aliuawa kwa kuchapwa risasi kwenye gari katika tukio la kufanana na Tupac. Baada ya nadharia lukuki na uchunguzi juu ya mauaji ya nguli hawa wawili, sasa huwenda tukaupata ukweli na kumjua muuaji wa Biggie.
Mwandishi wa Uingereza aitwaye Nick Broomfield anaamini ana ushahidi wa kutosha ambao unaweza kumtia hatiani muuaji wa Biggie. Kwenye Documentary iliyopewa jina la Last Man Standing: Suge Knight And The Murders Of Biggie & Tupac, Nick anasema askari polisi walihusika.
Aliendelea kudai kwamba kulikuwa na ufichwaji kwenye tukio zima na polisi wa Los Angeles kwa lengo kukwepa kulipa fidia ya nusu ya mabilioni ya Dola kwa familia ya marehemu Biggie. Anasema tukio hilo lilitawaliwa na rushwa, usiri na uhalifu wa kupoteza ushahidi. Aidha anaamini tangu dunia ishuhudie hukumu ya Derek Chauvin, askari polisi ambaye alihukumiwa miaka 22 jela kwa mauaji ya Mmarekani mweusi George Floyd, basi hata hawa waliohusika kumuua Biggie watawajibishwa.
from Author
Post a Comment